Doyo agoma kuutambua uchaguzi ADC

a Aziza Masoud,Dar es Salaam

ALIYEKUWA Mgombea wa nafasi ya Uenyekiti kupitia Chama Cha Alliance For Democratic Change (ADC) Doyo Hassan Doyo amesema kuwa hautambui uchaguzi wa viongozi  wa Chama hicho na kusisitiza kuwa ulienda kinyume na katiba na kanuni za Chama hicho.

Doyo ambaye katika uchaguzi huo alishindwa huku mpinzani wake Shabani Itutu akichukua nafasi hiyo alimtuhumu mwenyekiti mstaafu wa chama hicho Hamad Rashid Mohammed kuhodhi uchaguzi huo ikiwemo kuusimamia pamoja na kwamba hakuwa miongoni mwa wajumbe waliochaguliwa kusimamia.

Doyo ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam leo Julai 1,alisema hajaridhishwa na mwenendo wa uchaguzi huo kutokana na sababu mbalimbali  hivyo uchaguzi huo unapaswa kurudiwa  upya  ukiwa chini ya Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa na kwamba tayari ameshakata rufaa katika kamati ya uchaguzi ya Chama kama inavyoelekeza katika kanuni.

Akitaja sababu za kutokukubali uchaguzi  huo Doyo amesema Mkutano huo wa uchaguzi ulikwenda   kinyume na katiba na kanuni kutokana na kuongozwa na  Mwenyekiti Mstaafu  Hamad Rashid Mohammed  jambo ambalo ni kinyume na katiba na kanuni.

“Mwenyekiti Mstaafu Hamadi Rashidi Mohamed aliongoza mkutano kimakosa hivyo alivunja  kanuni zilizo kwenye katiba kwani katiba inasema Mkutano Mkuu wa Uchaguzi utaongozwa na Mwenyekiti wa muda atakayechaguliwa lakini haikuwa hivyo Mkutano ule uliongozwa na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Hamadi Rashidi Mohamed hoja yetu ya rufaa tunahoji kateuliwa na nani kuendesha mkutano ule na hakukua na tamko lolote” amesema Doyo

Pia amesema kuwa tayari wamepeleka rufaa ya kupinga matokeo hayo kutokana  na  mkutano  huo kuongozwa na Mwenyekiti  muda ambaye  anaeteuliwa kwa mujibu wa kifungu cha 10 cha Katiba ya chama.

“Mwenyekiti wa muda kwa mujibu wa kifungu hiki anatakiwa uchaguzi wa nafasi ya uchaguzi huo kitendo Cha Mwenyekiti anaemaliza muda wake Hamad Rashid mkutano mkuu wote Hadi chaguzi za makamu Mwenyekiti Kwa upande wa Bara na Zanzibar amevunja kanuni za Chama hivyo uchaguzi uchaguzi ni batili “ Amesema Doyo.

Aidha ameongeza kuwa taratibu za kupiga kura pia hazikuzingatiwa kwani wajumbe walikuwa wamezidi idadi inayotakiwa ambapo rejesta inayopelekwa kwa Msajili wa vyama vya siasa haikutumika kuongeza idadi ya kura za sheria 192 na kuwepo kwa kura 200.

Sambamba na hayo amesema Viongozi wapya wengi waliochaguliwa ni ndugu Mwenyekiti anaemaliza muda wake Hamad Rashid ambao amechagua mwenyewe hivyo inadhihirisha kuwa  anamaliza muda wake ila upande wa pili anakitaka Chama Kwa mgongo wa nyuma.

Hata hivyo Doyo amewashukuru Wapiga Kura 70 waliomwamini na kumpigia kura kati ya wajumbe halali 192 ambapo kwenye sanduku zilikutwa kura 200 ambapo kura hizo ni sawa na Kanda 7 kati ya 10.

Kwa upande  wake aliyekuwa Mgombea nafasi ya makamu mwenyekiti Zanzibar Shara Amrani Khamism amesema ajaridhishwa na namna uchaguzi ulivyofanyika kutokana na kuwa na chagamoto nyingi hivyo anaunga hoja zilizotolewa na Doyo.

Mwisho

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *