Wafanyabisahara wahimizwa kutumia fursa zinazotolewa na Korea

Na Aziza Masoud,Dar es Salaam

Katibu Mkuu wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Fatma Maborok Khamis amehimiza wafanyabiashara kutumia fursa zilizopo  kati ya Tanzania na Jamhuri Korea ili kufaidika na soko la bidhaa mbalimbali ambazo  nchi hiuo limeonyesha kuzihitaji  zaidi za nchini.

Akizungumza jana wenye maonesho ya 48 ya Kibiashara ya Kimataifa  ikiwa leo ni siku Maalum ya biashara ya Jamhuri Korea kama sehemu ya mwendelezo wa kutoa fursa kwa mataifa mbalimbali kuonesha biashara zao na tamaduni

 Amesema lengo  kuu  siku maalumu ya Jamhuri ya Korea  ni kuwakutanisha wafanyabiashara kati ya Tanzania  na Korea Kusini.

“Fursa kubwa kushirikiana suala muhimu kuweka  export  Tanzania na kampuni za Tanzania zina fursa  kupeleka bidhaa Jamuhuri ya Korea ikiwemo Korosho karafuu, chai  na kahawa,”amesema. 

 Amesema wameona Kampuni za Tanzania  zina fursa ya kujifunza  teknolojia ya kisasa kwenye uzalishaji  bidhaa  wameendelaea kwenye teknolojia.

Fatma ameeleza  kuwa  wafanyabiashara nchini  wanapaswa  kujifunza namna  gani wameweza kuboresha bidhaa katika teknolojia ya kisasa katika uzalishaji kuboresha thamani  ya bidhaa.

Amesema kuwa viongozi wanapaswa kuhamasisha wawekezaji kuwekeza Tanzania watanzania watakiwa  kuchangia mkia fursa zinazotengenezwa na viongozi. 

Amesema amewasikiliza wafanyabiashara wameeleza changamoto.m wanazokabiliana nazo ambapo yeye na Katibu Mkuu kuto bara watajadiliana kutatua changamoto hizo.

Akizungumza kwa Niaba ya Mkurugenzi  wa Mamlaka ya  Maendeleo ya Bisahara Tanzania (Tantrade),Meneja wa Masoko wa Ndani na Nje wa Tantrade  Dorothy  Urio amesema wadau kutoka Korea wanahitaji madini,korosho  na mengine kutoka Tanzania hasa kuboreshamnyororo wa thamani wa korosho.

Amesema  siku ya Korea  wamekuja na utamaduni wa Tanzania na Jamhuri ya korea kuonesha tamaduni mbalimbali ikiwemo kuonesha mavazi ya kiutamaduni.

Kwa upande wake Mshauri wa  Siasa na Uchumi kutoka Ubalozi wa Korea, Hyunseok Jeong amesema Leo ni siku muhimu  kwasababu  ni mara ya kwanza kushirikiana na Tantrade ikiwemo biashara na utamaduni.

“Inakumbukwa Juni mwaka huu Rais Dk.Samia Suluhu Hassan  Suluhu  alitembelea Jamjuri ya Korea hivyo uhusiano wa nchi hizi mbili  ni mzuri wataendelea kushirikiana na wafanyabiashara wa Tanzania na kubadilishana uzoefu,”amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *