Vituo vyakujaza gesi kwenye magari  zaidi ya 30 kujengwa Dar e s Salaam


Na Aziza Masoud,Dar es Salaam 

SERIKALI imesema inatarajia kuongeza vituo vya kujaza gesi asilia kwenye magari kutoka viwili  hadi vituo zaidi ya  30 vilivyopo mkoani Dar es Salaam ifikapo  mwaka 2025 ili kuwawezesha wananchi kupata huduma hiyo kwa uraisi.

Akizungumza leo Julai 9 katika banda la Shirika la Maendeleo Petroli Tanzania(TPDC)  alipotembelea katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa  maarufu kama Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam,Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba na kueleza kuwa lengo ni kupunguza foleni katika utoaji wa huduma hiyo.

‘Kupitia hotuba ya wizara ya Nishati na Madini iliyotolewa mwezi uliopita na waziri wa nishati iliweka vituo vingi vya kujaza gesi asilia kwenye magari,hivyo tutaongeza vituo hivyo jijini Dar es Salaam ambapo  kufikia mwaka kesho tunatarajia kuwana vituo zaidi ya 30 

‘Mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka huu tutakuwa tumejenga vituo maeneo ya Muhimbili,Kibaha,Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM),Sinza ,Mwenge,Goba ,Mbezi Beach na Mbagala,‘amesema Mhandisi Mramba.

Amesema kulingana na utaratibu  uliopo vituo hivyo vya kujaza gesi kwenye magari  baadhi vitajengwa na TPDC huku vingine vikitarajiwa kujengwa na sekta binafsi.

Amesema hata hivyo TPDC imejiongeza pamoja na kujenga vituo  kwa mfumo wa kawaida uliozoeleka pia wataleta magari ambayo yatauza gesi huku yanatembea.

‘Kwa hiyo gari itatoa huduma kwa mfumo wa  mobile  linaweza likafika mahali likaegesha  na kuanza kujaza gesi kwenye magari,hii ya kuwa na kituo kimoja tu cha Ubungo Maziwa  na cha Airport  tutaachana nayo ndani ya mwaka huu,‘amesema Mhandisi Mramba.

Amesema  mpaka mwakani  kutakuwa na magari mengi  yanaegesha huku akitolea mfano kuwa siku fulani wakiamua kuegesha Mwananyamala itakaa hapo na wateja wa maeneo hayo wataendana magari yao ili wajaziwe gesi.

Akizungumzia kuhusu bomba la mafuta la ECOP kutoka Ohima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga amesema mradi huo wa mafuta ghafi ratiba ya utekelezeaji wake unaendelea na kwamba kwa sasa umeshafikia asilimia 30.

‘Mpaka mwakani mwishoni mradi utakuwa umekamilika kulingana na ratiba ya mradi na hivi ninavyozungumza tayari kilomita zaidi ya 600 za mabomba zimetandikwa chini mambo yanaenda vizuri ila kwa sababu mabomba yapo chini hayaonekani yamefikiwa,’amesema Mhandisi Mramba. 

Amesema mpaka sasa mradi umeshafanyiwa usanifu,ulipaji fidia ambapo wamebaki watu wachache ambao wana mambo ya mirathi.

mwisho

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *