PURA kuongeza wawekezaji kwenye utafutaji gesi

Na Aziza Masoud,Dar es Salaam 

MAMLAKA ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imesema moja kipaumbele chao ni kuhakikisha wanaongeza  wawekezaji kwenye utafutaji wa gesi  

kwa  lengo la kuongeza matumizi ya gesi asilia viwandani na majumbani.

Akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kitaifa ya Dar es Salaam (DITF)  Mwenyekiti wa bodi ya Wakurungezi PURA, Halfani Halfani alisema kwa kipindi kirefu kumekuwa  hakuna uwekezaji wakutosha na  maeneo mengine hayana uwekezaji.

“Kisheria  wamerudisha yale maeneo serikalini hivyo tuna jukumu lakutafuya  wawekezaji ili kutekeleza hilo,taasisi imekuwa inafanya matayarisho ya   sheria,sheria ndogo inaelekeza wawekezaji watafutwe kwa ushindani sio kwakuokotwa hapana,”

“Ili  wapatikane kwa ushindani wanafanya mikutano yakutangaza marneo wawekezaji wanakuja wanasikiliza na wanaleta  propasal (dokezo) wa hayo maeneo,”amesema Halfani.

Amesema zoezi hilo huenda linaweza likafanyika  robo ya kwanza ya mwaka ujao

Alisema sheria ya mafuta inaelekea ni kazi ya waziri ni kutoa leseni  yeye ni mtoa leseni  hivyo anamwaga sera kama serikali alafu watalaam wanachukua jukwaa wanasema maeneo yaliyopo na masharti alafu itaamua nani atapata kitalu.

“Maeneo  ambayo yapo yanayozalisha gesi mpaka sasa Songosongo wilaya ya Kilwa  na Mnazi Bay wilaya ya Mtwara  vijijini lakini mwaka huu serikali imetoa leseni  ya uendelezaji ya pamoja kwa sababu ni uzalishaji,imetoa  kwa leseni kwa muwekzaji mmoja mwenye asili yakiarabu,”amesema.

Amesema mzalushaji huyo anategemewa kuanza kuzalisha gesi mwakani  hivyo sasa hivi atafanya matayarisho ya mwisho ambayo ni ujenzi wa bomba kutoka eneo la kisima mpaka kwenye  mitambo yakusafisha gesi Madimba.

“Tunategemea  atakuwa na uwezo  wakuzalisha takribani futi za ujazo milioni 100 kwa siku kiasi ambacho kinaweza kuongezeka  kadri gesi inavyoweza kuzalishwa na kadri visima vitakavyofanya kazi .

“Huyu muwekezaji atakavyoanza kuzalisha tutegemea  na hali ya uzalishaji kwa sababu  kwa kipindi cha muda mrefu tulikuwa tunategemea gesi ya baharini na gesi ya pale Lindi watatupatia zaidi kwa ajili ya matumizi ya majumbani,”amesema.

Amesema pamoja kwamba na watakuwa wanauza lakini kuna kiasi  fulani watatakiwa kukiacha hapa nchini .

“Hiyo ni kazi ya Pura kuhakikisha kunakuwa na ulinzi wa usambazaji,kama Pura tutajipanga vizuri ni lazima kuhakikisha hatutakuwa na uhaba wa gesi ,”amesema.

Mwisho

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *