Zaidi ya Wananchi 200  wataka kuunganishwa huduma ya Fiber Sabasaba

Na Aziza Masoud,Dar es Salaam

ZAIDI ya wananchi   200 wamewasilisha maombi katika banda ka Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL)  lililopo Viwanja vya Maonesho ya Mwalimu Nyerere maarufu kama Sabasaba kwa ajili yakuunganishwa na Fiber ya mtandao  wa intaneti  ambao ni nafuu zaidi.

Akizungumza katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Mkurugenzi  Mtendaji wa kampuni tanzu ya TTCL (T-PESA),Lulu  Mkudde amesema  katika  maonesho hayo wanafanya shughuli mbalimbali ikiwemo kuandikisha watu ambao wanahitaji mtandao wa intaneti majumbani ama fiber.

“Tumepokea maombi mengi wateja wanahitaji huduma hii ambayo imeleta mapinduzi,yale malalamiko ya vifurushi vya intaneti kuisha haraka hapa hayapo,shirika limeleta huduma hii kumuwezesha mwananchi kutumia Internet bila kikomo,”amesema.

Amesema kupitia mitandao  wamefungua  milango ya kidigitali kwakuweka mazingira wezeshi kwa wananchi katika kutumia huduma za Interneti katika kutekeleza huduma mbalimbali kwa wananchi. 

Akizungumzia kuhusu mkongo amesema mpaka sasa shirika linaendelea na mchakoto wa kufikisha huduma zake nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo ikiwa ni muendelezo wa kupeleka huduma hiyo kwa nchi za jirani. 

Amesema mpaka sasa huduma hiyo imefikishwa katika nchi nne ikiwemo Burundi,Rwanda,Zambia na Malawi.

Amesema  kwa Tanzania ,Shirika  limesambaza Mkongo wa Taifa katika mikoa yote nchini ambapo  zaidi ya wilaya 98 zikiwa nazo zimefikishiwa Mkongo wa mawasiliano.

Mkudde amesema juhudi hizo zote zinalenga kuhakikisha juhudi za huduma za Elimu, Afya na Maendeleo ya kiuchumi ambayo  yanatekelezeka kidigitali katika maeneo yote nchini.

Mwisho

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *