Na Aziza Masoud,Dar es Salaam
MAMLAKA ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli(PURA) imeweka malengo yakuhakikisha ifikapo mwaka 2034 matumizi ya nishati safi yakupikia kwa wananchi yafikie asilimia 80 ili kuweza kupunguza matumizi ya nishati ambayo inachafua mazingira.
Akizungumza katika jana Maonesho ya 48 ya Biashara maarufu kama Sabasaba Mkurugenzi Mkuu wa PURA Mhandisi Charles Sangweni alisema kutokana na ugunduzi wa gesi unaoendelea nchini wananchi wanapaswa kutumia nishati safi yakupikia.
‘Tumeweka malengo yakutumia nishati safi yakupikia kufikia asilimia 80 mwaka 2034 lazima,tutoke kwanye matumizi ya nishati ambayo inachafua hali ya hewa kama mikaa na kuni twende tukatumia nishati ambayo haina madhara kwa kiasi kikubwa,’alisema Mhandisi Sangweni.
Amesema wanafanya tunafanya tafiti mbalimbali zakuwezesha jambo hili liwezekane kwakuzalisha kiasi cha gesi ambacho kitaweza kuhudumia majumbani,katika magari na kwenye maeneo mengine.
Amesema mpaka sasa kuna maeneo ambayo tayari yameshagunduliwa gesi ikiweno Mnazi Bay pamoja na Songosongo iliyopo Mtwara.
Amesema shirika linaendelea na ugunduzi katika maeneo ambayo yana viashiria vya gesi ambapo imebainika ni asilimia 50 ya eneo la Tanzania.
‘Maeneo yenye viashiria ya mafuta SQM 5,034,000 karibu asilimia zaidi ya 50 za eneo la Tanzania,tushafanya tafiti SQKM laki moja elfu sitini na mia mbili,eneo tuliyofanyia utafiti mengi yapo Pwani kuanzia Kaskazini kwa maana ya Tanga,Kusini na Mtwara eneo hili limeenda mbali zaidi kuingia baharini zaidi ya km 400,eneo hili tulishapata kibali Umoja wa Mataifa (UN)na tushagawa katika vitalu,kwakuanza ukanda huu wa Pwani tutakuwa na vitalu ambavyo tutavitangaza,’amesema Mhandisi Sangweni.
Amesema kwasasa wanatangaza maeneo mbalimbali ambayo watavutia wawekezaji kwa ajili yakuja kushirikiana na taasisi pamoja na Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) kwenye kutafuta na ikiwezekana kinachopatikana wakiwekee mkakati wa kukiendeleza.