TBS YAFUNGUA DIRISHA LA TUZO ZA UBORA KITAIFA

Na Aziza Masoud,Dar es Salaam

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limetangaza awamu ya tano ya mashindano ya tuzo za kitaifa za ubora ambapo washiriki watashindanishwa katika  vipengele  vitano ikiwemo kipengele cha kampuni bora ya mwaka.

Akizungumza jijini leo  Agosti 14,Mkurugenzi  Mkuu wa TBS Dk.Ashura Abdul Katunzi amesema  tuzo hizo zilizoanza mwaka 2021 zina lengo  la kuwatambua na kuwapongeza watu binafsi  waliotoa mchango mkubwa  katika kuboresha miundombinu ya ubora au taasisi zinazofanya vizuri kwenye masuala  ya ubora wakati wa utekelezaji wa shughuli zao za uzalishaji bidhaa au utoaji huduma.

Amesema lengo jingine ni kuhamasisma ubunifu na uboreshaji    wa bidhaa na huduma zinazotolewa nchini kupitia taratibu  zilizowekwa chini ya miundombinu ya ubora.

Amesema tuzo za ubora kwa awamu ya tano kwa mwaka 2024 zimeandaliwa kwenye vipengele vitano ikiwemo tuzo za kampuni bora ya mwaka.

“Tuzo ya pili ni tuzo za bidhaa bora ya mwaka,tuzo ya tatu ni tuzo ya huduma bora ya mwaka ,tuzo ya nne    ya muuzaji bora bidhaa nje ya nchi,”amesema Dk.Katunzi.

Amesena  kipengele cha tano cha tuzo ni kwa mtu mkoha aliyefanya vizuri kwenye masuala ya ubora.

“Miongoni mwa vigezo vinanvyotumika kuwapata washindi ni pamoja na ni nini kinafanywa na taasisi husika au mtu binafsi kuongeza ubora wa bidhaa,huduma,ufanisi katika uzalishaji au utendaji  kazi kwa ujumla,”amesema Dk.Katunzi.

Amesema kigezo kingine ni  kwa kiasi gani taasisi au mtu binafsi anaweza kunufaika kwakuongeza ubora bidhaa,huduma au utendaji kazi,vile vile ni kwa namna gani biashara omekua baada yakuboresha bidhaa,hudima au uzalishaji  na utendaji kazi.

Naye Mkurugenzi wa Caps Tanzania Limited Peter Marealle ambaye kampuni yake inatoa huduma ya choo ambapo alipata tuzo ya huduma bora ya mwaka ya Jumuia ya Afrika Mashariki upande wa Huduma ya usafi wa mazingira,amewataka wafanyabiashara kushiriki tuzo hizo kwakuwa biashara zote zipo sawa.

“Hakuna biashara ndogo wala kubwa,wala biashara bora kuliko nyingine mfano sisi mtu anaweza  kusema biashara ya choo tu tumepata tuzo,lakini wanaangalia mifumo ya uendeshaji wa biashara na thamani ya fedha katika utoaji huduma hiyo,”amesema Marealle

Amesema thamani ya fedha inapimwa  na aina ya biashara  inayofanywa.

“Kampuni ikiendeshwa kimataifa gharama za uendeshaji zinakuwa ndogo tofauti na watu wanavyofikiri.

Upande wake Mtendaji wa Mkoa wa Pwani kutoka Chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo (TCCIA),Amilwise Mkayula  alisema watawashauri wajumbe wao na wanachama waweze kushiriki kwa wingi kwa sababu tuzo hizi zinafaida  katika kuendeleza biashara  zao na masoko yao.

”Hata walioshiriki mwaka jana wanaweza kushiriki tena kwa awamu nyingine,tunasisitiza kushiriki tuzo hizi kwani ndio itakavyoleta hamasa na ushindani mkubwa,”amesema.

Upande wake Mtendaji wa Mkoa wa Pwani kutoka Chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo (TCCIA),Amilwise Mkayula  amesema watawashauri wajumbe wao na wanachama waweze kushiriki kwa wingi kwa sababu tuzo hizi zinafaida  katika kuendeleza biashara  zao na masoko yao.

”Hata walioshiriki mwaka jana wanaweza kushiriki tena kwa awamu nyingine,tunasisitiza kushiriki tuzo hizi kwani ndio itakavyoleta hamasa na ushindani mkubwa,”amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *