Na Aziza Masoud,Dar es Salaam
MAMLAKA ya Mapato Nchini (TRA) imezindua Ofisi ya walipa kodi binafsi wenye hadhi ya juu ambapo kwakuanza wateja 158 wamekidhi vigezo vyakuhudumiwa wakiwemo wamiliki wa kampuni binafsi 111 zinazoingiza mapato ya Sh Bilioni 20 kwa mwaka.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ofisi hiyo iliyopo katika jengo la Golden Jubilee Tower,Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda amesema lengo la kufungua ofisi hiyo ni kuboresha huduma pamoja na kuwaomdolea usumbufu kundi hilo ambalo linaliingizia Taifa fedha nyingi.
“Huduma hiyo ya hadhi ya juu inatolewa kwa wamiliki wa kampuni ambao wanaingiza Sh Bilioni 20 kwa mwaka,wamiliki wa hisa katika makampuni amazo zina thamani ya zaidi ya Sh bilioni 2.5,mtu mwenye ubia na kampuni zinaingiza faida Sh Bilioni 20 kwa mwaka.
“Wale wote waliopata fursa zakuletwa gapa niwapongeze,wateja 111 wapo na sifa zakukaa kwenye kodi za juu zaidi na viongozi 47 nao wamo,nawahakikishia huduma zitakuwa bora zonazoendana na hadhi zao lakini pia itaondoa usumbufu,”amesema Mwendak.
Amesema kupitia huduma hiyo kwa sasa wameanza na walipa kodi 158 ambapo kati ya hapo wamiliki binafsi wapo 111 wote wameshaitwa kueleshwa kuhusu huduma hiyo,huduma pia itagusa viongozi wa mihimili mitatu ambapo kwa sasa viongozi 47 kutoka ngazi za juu,”amesema Mwenda.
Akitoa sababu zakuwahudumia makundi hayo amesema wamiliki binafsi wa kampuni mchango wao ni mkubwa sana kwa sababu wameanzisha kampuni,wameajiri watu wakati viongozi wamepewa kipaumbele hicho kwa sababu wana mchangi mkubwa wana majukumu mengi.