ULEGA:WATAFITI ACHENI KUZUA TAHARUKI

Na Aziza Masoud,Dar es Salaam

WAZIRI  wa Mifugo  na Uvuvi Abdalla Ulega amewataka watafiti  kushirikiana na wizara na taasisi mbalimbali pindi wanapohitaji kutoa matokeo ya tafiti zao ili kupunguza taharuki zinazotokea katika jamii pindi wanapotoa matokeo yao.

Ulega alitoa ushauri huo wakati akifungua  jukwaa la tasnia la kuku na ndege wafugwao ambapo alieleza kuwa hivi karibuni kulikuwa taarifa ya utafiti kuhusu wasiwasi wa ulishaji  kuku huku ikidaiwa kuwa na madawa  ambayo yanatumika kukuza kuku hao jambo ambalo lilizua taharuki.

“Natoa wito kwa watafiti kushirikiana na wizara ya mifugo wanapofanya tafiti zao ili kuepusha taharuki,hivi karibuni tulipata taarifa za kiutafiti walikuja kusema juu ya wasiwasi wao kuhusu ulishaji wa kuku,hii ilizua taharuki hivyo ni vizuri    tuwe tunawasiliana na tunapofanya tafiti kama hizi,”alisema Ulega.

Alisema serikali inawaheshimu  na kuwathamini watafiti kwakuwa lakini wanatamani wanapofanya tafiti kabla yakuzipeleka kwa walaji kuwe na mkakati wa pamoja wa jinsi yakuwasilisha taarifa kwa jamii.

Alisema tafiti ya namna ya namna  kuleta taharuki  na kusababisha watu kutokula nyama hivyo kuisababishia jamii kuwa na upungufu wa protini.

Amesema   asilimia 55 ya kaya Tanzania zinafanya  ufugaji kwakuwa mifugo haiitaji eneo kubwa.

“Kwa mujibu wa taarifa ifikapo 2030 nyama ya kuku itakuwa na uwezo wakuzalisha protini  kwa asilimia 41  ya protini itakanayo na wanyama,”alisema Ulega.

Alisema kutokana na umuhimu wa sekta ya kuku katika kufanikisha usalama wa chakula na ukuaji wa uchumi nchini  dhamira ya serikali ni  kuunga mkono sekta hiiyo kupitia miradi inayolenga vijana, ubunifu, na uendelevu.

Naye Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Shirika la Uboreshaji wa Kijana Tanzania (AGRA) Vianey Rweyendela  alisema lengo la majukwaa kama hayo ni kuhakikisha mkulima anaongeza tija.

“Tija ni ushindani wakulima ukiwauliza kuhusu bidhaa zai wanasema bei ni ndogo sokoni  bei haiwezi kuwa ndogo,lazima mkulima aongeze tija alafu anakuwa mshindani sokoni,”alisema.

Alisema katika jitihada zote hizi mdau  wa kwanza ni serikali  ambaye anatakiwa kumwekezesha mkulima pembejeo na kumsaidia mkulima katika masoko.

Mkurugenzi Mtendaji wa  Taasisi ya Inayojihusisha na Kukuza Kilimo Upande was Kusini mwa Tanzania (SAGCOT)  Geofrey Kirenga

Geoffrey Kirenga alitoa ujumbe wa kuhamasisha akitumia mfano wa Chips Mayai ili kuonyesha umuhimu wa kiutamaduni na kiuchumi wa bidhaa za kuku nchini Tanzania. 

Alisema, “Kuku ni chanzo muhimu cha lishe na kipato kwa maelfu ya familia. Tunapaswa kuendelea kuimarisha sekta hii kupitia ubunifu na uwekezaji.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *