SH BILIONI 600 KUGHARAMIA MIRADI MITATU BANDARI KIGOMA

Na Aziza MAsoud,Dar es Salaam

SERIKALI inatarajia kutumia Sh Bilioni 600 kwa ajili ya kugharamia miradi mitatu  itakayoboresha huduma ya usafirishaji wa majini mkoani Kigoma  na maeneo yanayozunguka.

Akizungumza  wakati wa kufungua  mkutano wa pili wa kimataifa was lojistiki na Uchukuzi,Waziri wa Uchukuzi Profesa Makamu Mbarawa      amesema miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa kiwanda cha meli,ujenzi wa meli ya mizigo pamoja na ujenzi wa meli ya kisasa ya abiria  inayotarajiwa kufanya safari zake katika ziwa Tanganyika pamoja Ziwa Victoria.

“Bandari ya Kigoma ni bandari muhimu kwa sababu kwenye ziwa Tanganyika tunapatkana na DRC  na kule kuna madini,Kigoma ni karibu  sana na Congo,kutakana na hilo serikali tukaona tuweke nguvu zakutosha  kuhakikisha tunatumia bandari ya Kigoma ipasavyo kujenga vyombo vya kisasa,”amesema Mbarawa.

Amesema kiwanda cha meli kinategemewa kujenga meli za kisasa huku ujenzi wa meli ya kisasa ya abiria inatarajiwa kubeba kati ya abiria 600 mpaka 900 wakati meli ya mizigo inatarajiwa kubeba tani 3000 ambapo itakuwa pia na njia za magari kwa mfumo wa mlango kwa mlango.

“Miradi hii yote ambayo itaanza hivi karibuni  itagharimu Sh Bilioni 600 ambapo itaboresha suala usafirishaji katika bandari ya Kigoma,”amesema Profesa Mbarawa.

Amesema kuna maendeleo mbalimbali yanaenda  kwa kasi kubwa,usafiri wa reli na majini.

“Haya ni mambo ya kawaida,kitu kikubwa zaidi kwa maendelo ya ziwa kujenga kwanza  meli ambayo itakuwa  na uwezo wakuhudumia  watu,kukamilika kwa ujenzi huu  wa meli kutaleta  ajira  kufungua sekta ya usafirishaji,kuleta ajira na kukuza uchumi,”amesema Profesa Mbarawa.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Chuo  Cha Usafirishaji (NIT)  Profesa Ulingeta Mbamba amesema  serikali imeandaa mkutano huo kwa ajili ya kuwakutanisha wataalam  wajadili kwakiasi gani nchi inaweza kupiga  hatua kwakufanya tafiti mbalimbali zakisafirishaji.

“Bila utafiti  hakuna suluhisho ambalo linapatikana kupitia chuo chetu tumekuwa tukitoa masuluhisho mbalimbali,”amesema Profesa Mbamba.

Kwa upande wa Mkuu wa Chuo cha NIT Dk.Prosper Mgaya  amesema kongamano hilo la siku mbili litajadili mbalimbali kuna mawasilisho ambayo yataletwa na watu wa taalum na mengine yataletwa na wataalam wa usafirishaji.

“Lengo la  kongamano hili tutoe mawazo ya kitaalam katika kuondoa katika mambo mbalimbali mfano waziri ameleeza pale kuhusu msongamano katika jiji la Dar es Salaam,”amesema.

Mwisho

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *