KAZI  250 ZAWASILISHA KAZI TUZO ZA SAMIA KALAMU AWARDS

Na Aziza Masoud,Dar es Salaam 

WASHIRIKI 250  kutoka mikoa 23 wamewasilisha kazi kwa ajili ya kushindania tuzo za ‘Samia Kalamu Awards’ zilizoandaliwa na Chama Cha Waandishi was Habari Wanawake nchini (Tamwa) na Mamlaka  ya Mawasiliano nchini (TCRA) ikiwa zimebaki siku sita kufungwa kwa zoezi hilo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Oktoba 24,Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa Dk.Rose Reuben amesema  kazi zilizowasilishwa zimetoka  katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam,Dodoma,Shinyanga,Mwanza,Mtwara,Simiyu,Geita,Njombe,Mbeya,Songwe,Rukwa.

Amesema kutokana na muitikio huo na umuhimu wa tuzo hizo  Tamwa na TCRA wameamkua kuongeza muda wa kuwasilisha tuzo hizo kutoka  Oktoba 23 mpaka 30.

“Uamuzi huu wa kuongeza muda umechukuliwa ili kutoa nafasi kwa wale waliokutana na changamoto za kiufundi, ikiwemo kushindwa kupandisha kazi mitandaoni, kutokana na matatizo ya mtandao na changamoto nyingine.

“Tuzo hizi zitatolewa kwa wanahabari wa Kitanzania, zikiwa na lengo la kuhamasisha, kukuza na kupanua wigo wa uandishi, utangazaji na uchapishaji wa maudhui ya ndani, kupitia vyombo vya habari vya asili na mitandaoni, ili kuchochea andishi wa makala za kina zinazozingatia maendeleo, uwajibikaji, mila na tamaduni pamoja na kujenga chapa na taswira ya nchi yetu,”amesema Dk.Rose.

Amesema hiyo fursa adhimu kwa vyombo vya habari, waandishi wa habari, na maafisa bari kuonesha umahiri wao wa kuchakata habari na kuthaminiwa kwa michango katika taaluma ya uandishi.

“Tunapenda kuwakumbusha kuwa kazi zinazowasilishwa zinatakiwa kuwa za kee na ambazo hazijawahi kuwasilishwa kuwania tuzo nyingine, na zinazofuata taratibu za haki miliki. Waandishi wanatakiwa kuwasilisha kazi zao kupitia tovuti rasmi ya www.samiaawards.tz,”amesema Dk.Rose.

“Tuzo za Samia Karamu Awards tumeongeza muda wa  kushiriki hadi Oktoba 30 awali ilikuwa Oktoba 26,uamuzi huu umetokana na watu kupambana na changamoto zakimtandao hasa wakupandisha kazi.

“Kwa taarifa hii tunawahamasisha wale ambao hawajawasilisha  kazi zao kuchukua hatua,kazi zinazowasishwa  kuwa zakipekee ambazo hazijawahi kuwaniwa sehemu nyingine,”amesema Dk.Rose.

Amesema mchakato wa upigaji kura utaanzia kwa wananchi utaanza rasmi Novemba nane mwaka huu.

 “Tunawahimiza wanahabari kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhim wa kushiriki katika upigaji kura kwa wingi, kwani kura za wananchi zinachangia asilimia 60 ya alama za mshindi, huku asilimia 40 zikiamuliwa na jopo la majaji. Wananchi wataweza kupiga kura kupitia namba maalumu ya SMS SHORT CODE 15200 au kwa kutumia tovuti rasmi,”amesema  Dk.Rose.

Naye Meneja wa Huduma za Utangazaji wa TCRA,Mhandisi Andrew Kisaka amesema  tuzo hizo ni muhimu kwa ajili ya kukuza na kutambua mchango wa waandishi wa habari katika masuala mbalimbali yakiwemo ya maendeleo.

“Tunaamini mna michango mizuri kwa jamii kupitia kazi zenu mlizozifanya kwenye redio, televisheni na mitandao ya kijamii. Nawahimiza kuziwasilisha kwa haraka katika kipindi hiki kilichobaki kwani tunaamini zimeleta mabadiliko chanya kwenye jamii,”amesema Mhandisi Kisaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *