WATANZANIA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA YAKUJIFUNZA USIMAMIZI WA MIRADI

Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam

BENKI ya Biashara Tanzania (TCB) imewataka watanzania ambao wapo katika taasisi mbalimbali  kujifunza kwa weledi usimamizi wa miradi ili kujua jinsi yakusimamia miradi kama ilivyo wataalam wa nchi za  nje ambao baadhi wamekuwa wakichukua tenda zilizopo nchini.

Katika sekta hiyo takwimu zinaonesha kuwa kwa mwaka jana, Afrika ilikuwa na chini ya mafunzo 10,000  ya uthibitisho wa usimamizi wa miradi, ikilinganishwa na Amerika ya Kaskazini yenye zaidi ya 40,000 na China ambayo iko juu ya 100,000.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji  benki ya TCB Allen Manzi, wakati wa kufunga kongamano la kukuza uelewa kuhusu usimamizi wa miradi kwa wataalam lililoandaliwa na Taasisi ya Usimamizi wa Miradi (PMI) upande wa Tanzania.

Amesema  TCB ikiwa kama mdhamini mkuu wa kongamano hilo imepata nafasi ya kuonyesha umuhimu wa usimamizi mzuri wa miradi jambo ambalo limekuwa changamoto kubwa kwa wataalam wa sekta hiyo nchini.

“Tunawaalika watanzania ambao wapo katika taasisi tofauti tofauti kuchangamkia fursa yakujifunza namna yakuendesha miradi, nchi za wenzetu wameichukulia hili kwa uzito mkubwa kwa sababu ya uelelewa wao na pia wamekuwa wanapata project (mitadi) nyingi katika nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania,”amesema Manzi.

Amesema endapo Watanzania watapata watajifunza sekta  hiyo watapata  fursa yakwemda kusimamia miradi nje kama nchi nyingine wanavyokuja kusimamiaTanzania.

Amesema  ujuzi wa usimamizi wa miradi unaweza kuathirika endapo taaluma hiyo haitazingatiwa kwa uzito.

Amesema kuwa TCB  imeamua kudhamini kongamano hilo ili kusaidia kuongeza uelewa kwa jamii na pia kuwakumbusha wataalamu ile miiko ya isimamizi wa miradi ili kuhakikisha thamani  ya mradi inaendana na  kila mradi inapatikana.

“TCB  inatoa wito kwa watu wote walioshiriki kongamano hilo kuhakikisha kwamba yale yaliyozungumzwa katika kongamano yanaongeza ufanisi kwenye utendaji kazi wao na kuongeza uelewa kwa wananchi,lakini pia washiriki hao waweze kuwa mabalozi wa namna ya utumiaji wausimamiaji bora wa miradi ambao utajikita kwenye kuhakikisha kwamba fedha zinazotumika kwenye mradi zinaleta tija iliyokusudiwa na pia maendeleo kwa jamii na nchi kwa ujumla” alisema Manzi

Naye Rais wa PMI upande wa  Tanzania, Kheri Mbiro, alisisitiza kuwa taaluma ya usimamizi wa miradi inapaswa kuingizwa kwenye mitaala ya elimu kama masomo mengine, jambo ambalo litaleta ufanisi zaidi katika utekelezaji wa miradi.

Aliongeza kuwa miradi inapaswa kufuata muda uliopangwa na kuhakikisha wanafunzi wanapata ujuzi wa kutosha, kwani kushiriki katika mafunzo haya ni njia mojawapo ya kujenga uwezo katika sekta hii.

Nafasi yetu kuhakikisha tunakuwa na watalaam wa kutosha na ili tuweze kusimamia miradi nje kwa sasa kunaonyesha kwamba kuna uhaba wa watalaam

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *