Na Mwamdishi Wetu,Dar es Salaam
SERIKALI imetoa msamaha wa kodi ya ushuru wa forodha (customs duty) asilimia 25 kwa injini za magari yanayotumia gesi asilia yanapoingizwa nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo Novemba 06,2024 Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Grace Tendega.
Tendega alitaka kufahamu mpango wa Serikali kupunguza baadhi ya kodi kwenye magari yanayotumia mfumo wa gesi ili Watanzania wengi waweze kuyaagiza.
Akijibu swali hiyo Kapinga amesema msamaha huo umetolewa kupitia Bajeti Kuu Serikali ya mwaka 2023/2024.
“Kupitia bajeti ya Serikali ya mwaka 2023/24 Serikali ilitoa msamaha wa kodi ya ushuru wa forodha (customs duty) asilimia 25 kwa injini za magari yanayotumia gesi asilia yanapoingizwa nchini,”amesema Kapinga