
WAANDISHI WA HABARI KUANZA KUJISAJILI KWENYE MFUMO WA TAI-HABARI – MSIGWA
Na Mwandishi Wetu, Shinyanga Serikali imesema vitambulisho vya Uandishi wa Habari (Press Card), vitaanza kutolewa wakati wowote baada ya siku saba kuanzia leo Mei 3, 2025 baada ya Waandishi wa Habari kuanza kujisajili rasmi kwenye mfumo wa TAI-Habari. Mwandishi wa Habari ataanza kujisajili kupitia kiunganishi cha https://taihabari.jab.go.tz kisha kufuata maelekezo yaliyotolewa ili kukamilisha kujaza fomu…