Na Asha Mwakyonde,DODOMA
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA),Dk.James Andilile
amesema kuwa wanajibidisha katika kuhakikisha huduma zinapatikana katika kiwango kinachotakiwa kwa wananchi ambao wana wahudumia.
Pia amesema EWURA kama taasisi za serikali na Utumishi wa Umma wanaendelea kusisitizana kutoa huduma katika viwango vinavyokubalika ili Rais Dk Samia Suluhu Hassan aweze kupiga hatua kiuchumi pamoja na kijamii na wananchi waweze kufurahia matunda ya serikali yao ambayo ipo madarakani.

Hayo aliyasema jana jijini hapa wakati akitoa maelekezo kwa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene alipotembelea banda la mamalaka hiyo katika maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2025 yenye Kaulimbiu isemayo ‘Himiza Matumizi ya Mifumo ya Kidijitali Kuongeza Upatikanaji wa Taarifa na Kuchagiza Uwajibikaji’.

Alisema kuwa EWURA kama moja ya taasisi za serikali wanameshiriki katika Wiki ya Utumishi wa Umma 2025 ambapo kimsingi wanalenga kuboresha huduma ambazo wanazitoa wa wateja wao.
Mkurugenzi huyo alieleza kuwa wao kama mamalaka inayohusika na masuala ya mafuta, maji, umeme pamoja masuala ya gesi asilia katika masuala ya udhibiti ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya serikali.
Dk.Andilile alisema kuwa huduma ambazo EWURA inazisimamia zinahusu watu huku akisema kama sehemu ya kuboresha utoaji huduma katika ushiriki wao kwenye maonesho hayo moja ni kuhudumia wananchi katika maonesho hayo.

“Hapa ninapoongea tuna mifumo yetu yote ambayo tunaitumia kufanya maamuzi ikiwamo mifumo ya Lois wananchi ambao wapo hapo wanaweza wakaja wakahudumiwa na timu yangu ya wataalam ambapo wapo hapa,” alisema.
Alifafanua kuwa hivi karibuni EWURA imeboresha mifumo ya utoaji huduma ili kuenfandana na kaulimbiu ya serikali ya wiki hiyo ya Utumishi huku akisema wateja wao wa leseni kwa sasa hawahitaji kwenda ofisini kupata huduma.

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA alisema huduma ambazo walikuwa wakizipata kutoka Kanda sita kwa sasa wanazipata kupitia mifumo ya Kidijitali na kwamba nia yao ni kuboresha mifumo kwa lengo la utoaji huduma.
“Kama sehemu ya kuchochea Uwajibikaji kwa taasisi ambazo wanazisimamia wamezitaka kuingia katika mikataba ya huduma kwa wateja na kwa sababu muda mwingine hawatoi huduma kwa wakati wamewaelwkeza kuhakikisha wanaweka website zao mikataba ya Huduma kwa wateja,” alieleza.
Kwa upande wake Simbachawene alisema ni vema mamalaka hiyo ikaangalia namna ya kurahisisha na kujumuisha usalama wa huduma.
