Na Asha Mwakyonde, DODOMA
MKURUGENZI wa Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Renatus Msangira amesema kuwa wakala huo itahakikisha inafikia malengo yote ya kuweka umeme vijijini ambapo kwa sasa wanaenda kuweka umeme kwenye vitongoji.
Pia amemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa malengo yake ya dhati ya kuhakikisha wananchi wote tanzania wanafikiwa na umeme pamoja na Nishati Safi ya kupikia.

Hayo aliyasema jana jijini hapa katika maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2025 yenye Kaulimbiu isemayo “Himiza Matumizi ya Mifumo ya Kidijitali Kuongeza Upatikanaji wa Taarifa na Kuchagiza Uwajibikaji” alisema wataifikisha huduma hiyo kwa wananchi wote.
Alieleza kuwa katika kuhakikisha azima ya Dk. Samia ya kuhakikisha matumizi ya Nishati safi ya kupikia inawafikia wananchi wote hivyo wakala huo wanahkiwa wananchi hao wanafikiwa na Nishati hiyo.
“Kama mnavyoona tunagawa majiko ambayo yanatumia uniti moja kwa saa, tunawakaribisha wananchi wote kuja kujionea shughuli zinazofanywa na REA kwenye masuala ya umeme vijijini katika masuala ya Nishati safi ya kupikia,” alieleza.

Mkurugenzi huyo alieleza kuwa wanamshukuru Rais Dk. Samia kwa malengo yake ya dhati ya kuhakikisha wananchi wote tanzania wanafikiwa na umeme.
Aliongeza kuwa lengo jingine la Dk. Samia ni kuhakikisha wanapata Nishati safi ya kupikia kwa wananchi wote.
Mkurugenzi huyu alisema kuwa hivi karibuni wametekeleza mpango wa taasisi za Umma kuhakikisha taasisi zote zinatumia Nishati hiyo ya kupikia huku akisema wanampango wa kushirikiana na Ofisi ya Rais Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), kzifikia taasisi zote zilizopo chini ya Wizara hiyo zikiwamo shule, hospitali pamoja zile zenye my watu wenye kuanzia 100.

Aidha aliwakaribisha wananchi wote wa Mkoa wa Dodoma na nje ya Mkoa huo kutembelea wiki hiyo ya Utumishi wa Umma na kujionea huduma mbalimbali zinazofanywa na Wakala huo.
