Na Asha Mwakyonde, DODOMA
WIZARA ya Katiba na Sheria imepongezwa kwa ufanyaji kazi katika Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC), ambao umerahisisha mambo na kufungua maendeleo.
Hayo yalisemwa jana jijini hapa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene wakati alipotembelea banda la wizara hiyo katika maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2025 yenye Kaulimbiu isemayo “Himiza Matumizi ya Mifumo ya Kidijitali Kuongeza Upatikanaji wa Taarifa na Kuchagiza Uwajibikaji” alisema kuwa kujua maendeleo yanapatikana lazima migogoro iondolewe.

Alisema kuwa sehumu kubwa ya mambo ambayo walikuwa wakiyafanyia kazi ni yale ya migogoro huku akisema kama ni kesi tayari zilikuwepo mahakamani.
Waziri huyo alifafanua kuwa migogoro kuibalisha kwenda kwenye kesi huwa ni shida
“Mefanya vizuri kiukweli mmemsaidia muheshimiwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha Taifa linakuwa na watu wenye upendo na amani huku akisema migogoro inaleta chuki na kiumizana,” alisema Simbachawene.
Aidha aliitaka wizara hiyo kuendeleza kampeni hiyo kwa kuw imesaidia kupunguza gharama na kuzifanya familia kuendeIea kuwa na utulivu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka wizara ya Katiba na Sheria Mbaraka Stambuli alisema kuwa kampeni hiyo hadi sasa imefika katika mikoa yote ya Tanzania Bara na kwamba imeshafika Zanzibar mikoa mitano.
“Takribani wananchi milioni 3 wameshafikiwa na kampeni hiyo Tanzania Bara na Zanzibar hii ni awamu ya kwanza ya utekelezaji na utoaji wa haki ni jambo endelevu kampeni hii itaendelea kutekelezwa tena ili kuimarisha zaidi huduma za kisheria,” alisema.
Awali Wakili wa serikali kutoka wizara hiyo Athumani Mososole
alisema kuwa wizara imekasimiwa mamalaka ya kutekeleza Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC), yenye lengo la kutoa elimu kwa wananchi masuala mbalimbali ya kisheria pamoja na utawala bora.

Alisema kuwa wizara inakituo Cha huduma kwa wateja ambacho kinasikiliza malalamiko ya wananchi na kuweza kutoa ufafanuzi siku zote za kazi kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa.
