MAWAKILI WA SERIKALI KUKUTANA DAR KESHO

Na Aziza Masoud Dar es Salaam

MAWaKILI wa Serikali  nchini wanatarajia kukutana kesho jijini Dar es Salaam kupitia kongamano lenye lengo la kuwaunganisha na kutoa elimu kwa jamii katika masuala mbalimbali yakijamii.

Katika kongamano hilo  mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dk.Jakaya Kikwete unatarajiwa kuhudhuliwa na mawakili kutoka Tanzania Bara na Visiwani.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Juni 20, 2023. Rais wa Chama Cha Mawakili wa Serikali Tanzania Bavoo Yunus  amesema kongamano hilo lina lengo la kuwakutanisha mawakili hao pamoja ili  kuweza masuala mbalimbali yakijamii.

“Lengo letu ni kuwaletama mawakili  pamoja kuweza kujadili masuala mbalimbali yanayotuhusu jamii,pia tunatumia kongamano hilo kama jukwaa lakutoa elimu na mafunzo kwa wananchi  kwa sababu sisi ni watumishi wa serikali na serikali inawajibiika kwa wananchi,”amesema Yunus.

Amesema mawakili wa serikali wanatakiwa  kuhakikisha elimu katika masuala ya kisheria hususani  masuala mapana yakisheria.

“Katika kutekeleza wajibu huu chama kimeona ni busara kikaandaa kongamano kwa ajili ya kuelimisha masuala haya,”amesema Yunus.

Amesema katika kipindi chakuelekea uchaguzi mkuu ni wajibu wa wanasheria kuhakikisha  wananchi wanajua sheria na kutambua  umuhimu wa amani ili wafahamu tofauti zakichama zisiharibu umoja katika nchi.

“Lengo uchaguzi ufanyike  kwa amani tofauti zetu zisifunge umoja wetu,katika jamii yetu mambo yanayotuuunganisha ni makubwa,mengi na mazito kuliko yale yanayotutofautisha,”amesema Yunus.