KEKI KUBWA ZAIDI AFRIKA MASHARIKI YATINGISHA SABASABA

Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam

KATIKA Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama sabasaba,kampuni ya Laziz Bakery imeibua mshangao na kuvutia maelfu ya watazamaji baada ya kutengeneza keki kubwa yenye uzito wa tani 3 sawa na kilo 3,000 ikiwa ni keki kubwa zaidi kuwahi kutengenezwa Afrika Mashariki.

Keki hiyo si tu ya kipekee kwa ukubwa wake bali pia kwa ujumbe wake  imebeba taswira ya uzalendo na kuakisi miradi mikubwa ya uwekezaji inayotekelezwa na Serikali ya Tanzania katika sekta mbalimbali kama vile miundombinu ya Barabara , afya, elimu na viwanda. 

Akizungumza Katika Maonesho hayo yanayofanyika Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya LAZIZ BAKERY limited, Hamza Muzammil  ameeleza kwamba ubunifu huo umelenga kuonyesha maendeleo yanayopatikana chini ya mazingira bora ya biashara na  uwekezaji  yaliyowekwa na serikali ya awamu ya sita.

“Keki nimeitengeza kwa siku 15,na ina uwezo wakukaa  kwa muda wa siku 12,keki inayoonyesha miradi mbalimbali iliyotekelezwa na serikali,zaidi ya miradi mikubwa kumi ipo hapa,”alisema Muzzammil.

Alisema  Tanzania imekuwa nchi bora katika uwekezaji suala ambalo linasababisha na wao kuweza kufanya biashara kwa utulivu na ustaarabu.

“Nchi hii inatupa kila siku tunakuja kufanya biashara bila shida serikali inatusapoti sanaSabasaba tunakata ili kila mtu apateuwekezaji Tanzania upo vizuri ,kila mtu anaweza kuja kuwekeza hakuna shida,serikali imeweka mazingira rafiki,”alisema.

Kwa upande wake Balozi wa bidhaa za vyakula zinazotengenezwa la Kampuni hiyo ikiwemo keki, Burton Mwemba maarufu kama Mwijaku amebainisha kwamba ubunifu wa kuweka Miradi mbalimbali ya maendeleo inayofanywa na serikali nchini Katika keki hiyo kubwa ni ishara ya kuunga mkono jitihada za serikali katika kukuza uchumi na kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Aidha, ameeleza kuwa hatua hiyo ni  mfano bora wa namna sekta binafsi inaweza kushirikiana na serikali katika kuhamasisha maendeleo na uwekezaji ndani nchi.