Na Aziza Masoud, Dar es Salaa.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi ameipongeza Shirika la Bima Taifa(NIC)kwa uanzishwaji wa Bima ya maisha (BeamLife) ambayo wahusika wanaweza kuchangia Sh 5000 kwa mwezi.
Akizungumza hayo jana jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea banda la NIC katika maonesho ya Kimataifa ya 49 ya Biashara ya Dar es Salaam(DTIF) maarufu lama Sabasaba,P alisema bima hiyo inamanufaa makubwa kwa makundi mbalimbali ikiwemo wakinamama hivyo amesema kuna haja ya yeye kuipeleka jimboni kwake na kuihamasisha.

“Nimeambiwa hii ni bima inayotoa riba shindani kwa fedha zilizowekezwa kidogo kidogo au kwa mkupuo hususani kwa wananchi wenye vipato cha chini.,”alisema Profesa Kabudi.
Alisema huduma ya bima hiyo anaamini itakuwa mkombozi hasa kwa wananchi wa kipato cha chini.
”Awali nilikuwa mteja wa bima ya maisha katika Shirika hili lakini tayari umri wangu umevuka wa kuwa na sifa hiyo,kwahiyo sasa hivi siruhusiwi tena ila kikubwa nimefurahia Bima ya BeamLife.

”Ni muhimu sana kuelimisha watu kuhusu bima hii kwani ni 5000 kwa mwezi na kwa mwaka ni kama 60000,ni nzuri sana kwa watu wa chini,”alisisitiza Prof.Kabudi.
Awali akielezea Bima hiyo,Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa NIC,Karim Meshack alisema kwa kujiunga na bidhaa ya bima hiyo mteja anapata faida inayotokana na uwekezaji wa masoko ua fedha na mitaji huku akinufaika na huduma za ziada za rambirambi kutokana na kifo kinachoweza kutokea kwa mke,watoto au yeye mwenyewe.

Alisema kiwango cha chini cha kuchangia bima hiyo ni kiasi cha Sh.5000 na endapo mteja ataweza kuchanga kwa mkupuo ataweza kuchanga kwa kiwango cha chini ya Sh. 2,000,000.
”NIC inabima za aina mbalimbali ambazo tunatoa kwa huduma bora unaostahili,kwa sasa huduma zetu tunaziendesha kidigitali sio lazima mteja aje katika banda letu au Ofisini anaweza akawa huko huko na akafanya maombi yake kiganjani.

”Na kupitia kidigitali unaweza kuomba madai ukafatilia na kuyaandikisha na kufatilia madai na kisha kupatiwa majawabu ya moja kwa moja katika maombi yako,”alisisitiza Meshack.
Alisema bima hiyo ya BeamLife inalenga watu wa kipato cha chini wakiwemo madereva wa bodaboda kutokana na kima chake cha mwezi kuwa kidogo na kufanya mwanzo wa maisha kuwa mzuri.

