Na Aziza Masoud,Dar es Salaam
MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imewataka wahitimu wa shule za sekondari pamoja na wafanyakazi waliopo viwandani kujiunga na chuo hicho kusomea kozi zakuendesha mitambo na machine za viwandani.
Akizungumza leo Julai 4, ,2025atika Maonesho ya Biashara ya 49 ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DTIF) maarufu kama Saba Saba Mkufunzi Kutoka Veta tawi la Kipawa Joshua Mwankusye alisema mamlaka inatoa mafunzo ya mifumo yakuendesha mashine ziweze kufanya kazi wenyewe.

“Kuna kozi fupi kuna system ya mifumo yakuendesha mashine zifanye kazi zenyewe kwa msaada kidogo,ni kozi ya muda mfupi wa miezi miwili anakuwa qualified baada ya hapo ataenda field viwandani kwa ajili yakuboresha alichojifunza,”alisema Mwankusye.
Alisema kozi hiyi kwa VETAni muhimu kwakuwawat7 wengi huwa wanaenda kuisoma nje ya nchi tena kwa gharama kubwa tofauti na VETA ambapo inapatikana kwa gharama nafuu.
“Wengi waliokuja ni tayari wameshapata kazi,muitikio wa wanafunzi bado mdogo kwakuwa wazazi kwakuwa bado hawajaelewa vizuri tunapowaambia kozi itawasaidia kupata ajira na kujiajiri,*alisema.

Alisema mpaka sasa jumla ya wanafunzi 35 wameshahitimu kozi hii tangu ilipoanzishwa mwaka juzi .