Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam
MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo Stadi (VETA) imeanzisha kampuni tanzu ambayo inahusika na kukuza bidhaa bunifu zinazotengenezwa kupitia vyuo vyake mbalimbali.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurungezi Mkuu wa VETA, Anthony Kasole wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya 49 ya Kimataifa ya kibiashara Sabasaba yanayoendelea.
CPA Kasole alisema VETA imeanzisha kampuni hiyo ambayo inahusuka na kukuza bidhaa bunifu zinazotegenezwa kupitia vyuo vyake mbalimbali .

“Bidhaa zote ambazo zitakuwa zikitegenezwa na wanafunzi kutoka katika vyuo hivyo zitakuwa zikiuzwa katika Kampuni hiyo tanzu,”
Alisema kampuni hiyo tanzu itakuwa ikihususika na bidhaa zote tunazozitegeneza pamoja na kutoa huduma mbalimbali kuanzia katika eneo la utengenezaji fanicha na usimamizi wa miradi.
Katika hatua nyingine CPA Kasole amesema inajivunia mageuzi makubwa iliyoyafanya katika sekta ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi nchini ambayo yamewezesha Watanzania wengi kujiajiri na kuajiriwa.
“Kwa sasa VETA tunatoa ujuzi katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwa wale watu wanaohudumia wazee .majumbani , takribani watu 700 wameweza kuhitimu mafunzo na kupata ajira”amesema CPA Kasole

Aidha amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kuweza kuweka msisitizo katika elimu ya mafunzo na Ufundi stadi .
Amesema kupitia msisitizo huo VETA wameweza kuona manufaa makubwa sana na kuweza kufaidika na kutekeleza mambo mengi .
“Kwa sasa VETA ina vyuo 80 nchini na 65 vinakwenda kumaliziwa na Serikali…Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa fedha kwa ajili ya ujenzi vyuo hivyo ambao upo katika hatua nzuri ya ukamilishaji wa awamu ya kwanza”amesema
Mkurungezi Mkuu huyo amesema kukamilika kwa vyuo hivyo VETA itakuwa na jumla 145 hapa nchini katika kila wilaya ambayo vinakwenda kuwasaidia wananchi kupata elimu na ujuzi wanaotaka Kwa urahisi.
