Na Aziza Masoud,Dar es Salaam
MAMLAKA ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), ipo katika maandalizi wa uchimbaji wa visima vitatu vya gesi asilia mkoani Mtwara kwa lengo la kuongeza zaidi uzalishaji wa nishati hiyo
Akizungumza leo Julai 9, 2025 na Mkurugenzi Mkuu wa PURA na Mhandisi Charles Sangweni alipotembelea katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam(DITF) maarufu lama Saba Saba alipotembelea katika banda la PURA na taasisi nyingine zinazohusiana na wizara ya nishati.

Alisema kwa sasa wapo katika mchakato wa kuchimba visima vitatu vya gesi asilia mkoani Mtwara unaotarajia kuanza Novemba mwaka huu.
“Sasa hivi kuna kampeni ambayo ipo kwenye maandalizi tutachimba visima vitatu Mtwara lakini katika ile block Tanzania tunashiriki kwa asilimia 50,visima hivi vinatarajiwa kuongeza uzalishaji wa gesi asilia nchini.
Alisema katika uchimbaji huo Shirika la Petroli Nchini (TPDC )limeshiri kwa 40% huku asilimia 60% zilizobaki zinafanywa na kampuni ya nje ya nchi”amesema.

Aliongeza kuwa katika makampuni kumi ambayo yanapatiwa tenda ya kufanya kazi kwenye miradi hiyo,PURA itahakikisha zaidi ya kampuni sita zitakuwa za kitanzania ili kuhakikisha watanzania wanafaidika na miradi hiyo.
“Kazi zote ambazo zinaweza kufanyika kwa makampuni ya kitanzania zinafanywa na Watanzania kwakuwa sasa hivi kumekuwa na jitihada kubwa ya serikali kuhakikisha wanapata watalaam wa masuala ya mafuta na gesi ikiwemo kuanzisha kozi z masomo hayo,”alisema Mhandisi Sangweni.
