Na Mwandishi Wetu,Morogoro
UONGOZI wa Website ya Taifa Tanzania inaomba radhi kwa stori iliyochapishwa Julai Mosi yenye kichwa cha habari ‘Wajumbe wa CCM Morogoro walizwa kwa kigezo cha zawadi kwa Ally Happy’ kwakuwa stori hiyo ilinukuliwa vibaya.
Katika stori ambayo ilidaiwa kuwa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) wilaya ya Morogoro kuwa imechangisha michango kwa kigezo cha zawadi kwa Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Ally Hapi.
Kwa mujibu wa watoa taarifa ambao hawakutaka kutajwa majina walidai kuchangishwa kiasi cha Sh 20,000 kutoka kila Kata ili kumuandalia zawadi Happi ambaye alitarajiwa kufanya ziara Mkoani Morogoro.
Walieleza maagizo hayo walipewa kupitia kikao cha Baraza la Jumuiya ya Wazazi wilaya, kilichoitishwa Juni 18 Mwaka huu, katika ukumbi wa Halmashauri, wajumbe hao kutoka kila Kata ambao ni Mwenyekiti, Katibu, Malezi pamoja na Mjumbe wa Halmashauri Kuu kila mmoja alipewa agizo la kuchanga kiasi Sh 5000 kwa ajili ya zawadi hiyo kupitia Katibu wa Jumuiya wa Wazazi Wilaya Emmanuel Nestory Icon.
Baada ya kufuatilia tumegundua kuwa habari hiyo ilikuwa na mapungufu yakitaaluma hivyo uongozi unaomba radhi kwa usumbufu uliojitikeza.