UCHAGUZI MKUU KUFANYIKA OKTOBA 29, KAMPENI KUFANYIKA KWA MIEZI MIWILI

Na Asha Mwakyonde, DODOMA

TUME ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), leo imezindua Kalenda ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2025, Oktoba 29, 2025 Siku ya Jumatano Itakuwa ndiyo Siku ya Kupiga Kura
huku ikiwataka wadau wote ikiwa ni pamoja na wananchi kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi kwa kuzingatia sheria, kanuni, miongozo na maelekezo yatakayotolewa na Tume hiyo.

Akizungumza leo Julai 26,2025 jijini hapa Mwenyekiti wa INEC ,Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele mara baada ya uzinduzi huo
amesema Tume hiyo kwa mamlaka iliyonayo chini ya ibara ya 41(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ikisomwa pamoja na kifungu cha 49(1)(a) na 68(1) vya Sheria ya Uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani Namba 1 ya mwaka 2024 inatangaza Ratiba ya Uchaguzi wa Rais na Wabunge katika Jamhuri ya Muungano na Madiwani kwa Tanzania Bara mwaka 2025.

Jiji Mwambegele ratiba ya uchaguzi wa Rais na wabunge katika Jamhuri ya Muungano na madiwani kwa Tanzania Bara mwaka huu kwamba Agosti
09, hadi Agosti 27 mwaka huu Itakuwa utoaji wa Fomu za uteuzi wa wagombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais.

Ameeleza kuwa Agosti 14, 2025 hadi Agosti 27 Itakuwa utoaji wa fomu za uteuzi wa wagombea Ubunge na Udiwani na huku akifafanua kwamba Agosti 27 mwaka huu itakuwa siku ya Uteuzi wa Wagombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais, uteuzi wa wagombea Ubunge na uteuzi wa wagombea Udiwani.

“Tarehe 28 Agosti, 2025 hadi tarehe 28 Oktoba, 2025 Kitakuwa kipindi cha Kampeni za Uchaguzi kwa Tanzania Bara,” amesema Jiji Mwambegele.

Ameongeza kuwa Agosti 28, hadi Oktoba 27 mwaka huu ni Kipindi cha Kampeni za Uchaguzi kwa Tanzania Zanzibar ili kupisha kura ya mapema na Oktoba 29 , 2025 Siku ya Jumatano Itakuwa ndiyo Siku ya Kupiga Kura.

Awali Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo ya Uchaguzi Ramadhani Kailima ameeleza kuwa kwa kuzingatia matatwa ya kifungu Namba 16 kifungu cha 5 cha sheria ya uchaguzi wa Rais na madiwani Namba 1 ya mwaka 2024 Tume imekamilika uboreshaji wa daftari la mpiga kura awamu mbili katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR MAGEUZI, Ndg. Evelyn Munisi amesema kuwa wao baada ya kipenga cha Kalenda ya Uchaguzi kutangazana Tume hiyo wanaenda kujipanga vizuri zaidi ya mwanzo huku akisema tayari Chama hicho kimeshamchangua mgombea nafasi ya urais pamoja na mgombea mwenza.

Amesema Chama hicho tayari kimeshapata watia nia wa majimbo zaidi ya 200 na madiwani huku akisema kwenye uchaguzi huo NCCR MAGEUZI wapo vizuri.

Munisi ameongeza kuwa wana imani na Tume hiyo ambapo haijawaacha nyuma vyama vya siasa imekuwa nao bega kwa bega kwenye kila hatua.

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha National League for Democracy (NLD), ambaye pia ni mgombea nafasi ya urais katika Chama hicho Doyo Hassan Doyo, ametoa pongeza kwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mwambegele kwa kuwapatia mwaliko wa kushuhudia uzinduzi wa Kalenda ya Uchaguzi mwaka 2025.

“Tukio la leo ni kubwa na la kihistoria pia naipongeza Tume hii ya INEC pamoja na Mwenyekiti wake Jaji Mwambegele tukio hili huko nyuma lilikuwa likifanywa na waandishi wa habari wakiwa ofisini kutangaza taarifa ya uchaguzi lakini kipindi hiki wameona watumie busara kubwa ya kuwashirikisha,kuwaalika wadau mbalimbali,” amesema.

Aidha ameeleza kuwa amewahakikishia watanzania kwamba wanaenda kushiriki uchaguzi huo wakianini Tume hiyo ina kwenda kutenda haki katika yale ambayo wamekusudia kuyafanya katika uchaguzi.