RAIS DK.SAMIA KUZINDUA KITUO CHA BIASHARA EACLC IJUMAA

Na Aziza Masoud, Dar es Salaam

RAIS Dk.Samia Suluhu Hassan  anatarajiwa kuzindua Kituo cha Cha Biashara na Usafirishaji cha Afrika Mashariki (EACLC)  kilichopo Ubungo kesho ambapo kina maduka 2000 ya biashara pamoja na miundombinu nyingine.

Akizungumza jijini  leo Julai 30, 2025,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila alisema kituo hicho kilichojengwa na serikali kwakushirikiana na sekta binafsi kampuni kutoka China kimejengwa wa gharama za Dola za Marekani Milioni 100(Sh Bilioni 282.7) kitazinduliwa  na Rais Dk.Samia  kutokana na ukubwa na heshima ya kituo hicho.

“Rais Dk.Samia ametupa heshima kuja kuzindua kituo hiki Agosti  Mosi,serikali inawaalika wafanyabiashara wote watanzania na wasio watanzania kuja kufanya biashara kwakukodisha maeneo ya biashara katika sehemu hiyo,”alisema Chalamila.

Alisema siku ya uzinduzi huo wafanyabiashara wote waliochukua maeneo hayo watakuwepo katika sehemu zao biashara. 

“Tunategemea kuwa na wafanyabiashara waliochukua na wanaotegemea kuchukua maduka watakuwepo katika uzinduzi huo,”alisema Chalamila.

Alisema  kituo hicho chenye maduka maduka 2000,sehemu yakuegesha magari,sehemu za ofisi ambazo zote zinakodishwa kwa lengo la kufanya biashara.

Alisema kituo kilianza kujengwa Mei 2023  kimekamilika na kuna maduka zaidi ya 2000 pamoja na miundombinu nyingine.

“Kituo kimejengwa kwa zaidi ya Dola Milioni 100,uwekezaji huu ni miongoni mwa uwekezaji wakimkakati uliofanywa na wawekezaji na manispaaa kujengwa na wawekezaji kutoka China,ni mfumo tu wa ubia kama miradi mingine kwa mustakabali wa uchumi wa nchini,.

“Miradi kama hiyo  DDC Kariakoo,Mlimani City ujenzi huu sio jambo jipya ndani ya Taifa letu,tunawakaribisha ili tuweze kufanya biashara ndani na nje ya nchi waje kufuatilia kupitia kituo cha uwekezaji,”alisema Chalamila