TUME YA MIPANGO YATAKA SERA,SHERIA ZINAZOENDANA NA DIRA 2050

Na Aziza Masoud,Dar es Salaam
TUME ya Taifa ya Mipango (NPC) imesema miongoni mwa vitu ambavyo wataviangalia kwa ukaribu ni sera na sheria za nchi ziweze kuendana na Dira ya Taifa 2025-2050 ili kuweza kutekeleza mpango huo kama inavyotarajiwa.

Kauli hiyo imetolewa leo Agosti 19, 2025 na Naibu Katibu Mtendaji anayeshughulikia Mipango ya Kitaifa wa Tume yaTaifa ya Mipango Dk.Mursali Milanzi wakati wa semina kuhusu kwa waandishi wa habari iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) alisema lengo la serikali ni kuangalia namna nzuri yakutekeleza dira hii kupitia Tume.

“Tunataka kuangalia ni namna gani serikali kupitia Tume ya Mipango inajiandaa kutekeleza dira kupitia mifumo mbalimbali kwakuangalia masuala mbalimbali hasa kangalia upya kwa sheria na sera ili tuone hivyo hivyo vitu viendane na dira,”amesema Dk.Milanzi.

Akizungumzia kuhusu utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025-2050,Dk.Milanzi amesema tume inafanya jitihada mbalimbali hasa kuelimisha jamii kuhusu malengo yaliyotengenezwa na kuyasimamia kwa lengo la kuhakikisha wanabadilisha fikra za watu na kuacha habari za mazoea.

“Tunataka kubadilisha fikra zetu tuachane na mambo ya mazoea,tuaipofanya hivyo hatuwezi kufikia malengo,watu waache kufanya kazi kawaida ili baada ya miaka 25 tusije kukutana kwenye kikao kama hiki mwaka 2050 na kugundua kuwa hatujafanya kitu,”amesema Dk.Milanzi.

Amesema kwa upande wao tume kama jukumu lao lakusimamia dira hiyo lilivyo hivyo wataenda tofauti na utaratibu wa kawaida ili waweze kufikia malengo.

“Tume tutaweka mbele vipaumbele vyenye tija na kutekeleza malengo ya dira ili yale tuliyoyapanga yafikiwe hivyo ni jukumu la waandishi wa habari kuwasaidia wananchi kuihoji serikali kuhusu mwelekeo wa dira baada yakupata elimu kuhusu dira,”amesema Dk.Milanzi

Amesema ni wakati wa wanahabari kushirikiana na tume kutoa elimu ili kila mwananchi aone mchango wake katika kutekeleza dira hii hivyo kila mmona anapaswa kuielewa.

Naye Afisa Mwandamizi wa UNFPA Kitengo cha Idadi ya Watu na Maendeleo Samwel Msokwa alisema shirik hilo limekuwa likishirikiana na serikali katik kutengeneza mipango mbalimbali ya maendeleo pamoja na uzalishaji takwimu data.
“Lengo la warsha hii ni kutoa elimu wa kundi la wabahabari ili waendelee kuelimisha wananchi kuhusu dira,tunategemea elimu hii itaendelea kwa jamii ili waweze kujua nafasi yao katika utekelezaji wa dira hii,”amesema Msokwa.

Amesema maendeleo ni pamoja na mipango na uzalishai wa takwimu na data ambazo zitasaidia kupanga mipango.