Mwandishi Wetu,Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa,Mohammed Ali Kawaida (MCC) amezindua Mfumo wa kisasa wa Kijani Ilani Chatbot ambao utaenda utawarahisishia vijana kufahamu mambo yaliyofanywa na serikali 2020-2025 na yanatarajiwa kufanywa 2025-2030 kupitia CCM kwakutumia vifaa vya mawasiliano popote alipo.
Akizungumza wakati wa Uzinduzi huo uliofanya jana jioni Jijini Dar es Salaam, Kawaida amesema uzinduzi Kijani Ilani Chatbot sehemu ya kuwaonyesha vijana wa kitanzania na watanzania wote ni namna gani vitu vyote vilivyoahidiwa na chama vinavyotekeleza katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Kijani Ilani Chatbot itakwenda kutuonyesha ilani yetu ya uchaguzi ya mwaka 2025-2030 vitu gani imehahidi hususani kwa upande wa vijana wa kitanzania na kuonyesha kitu gani chana kimetekeleza kupitia ilani inayomalizika mwaka huu,” amesema Kawaida.
Aidha amewasihi vijana kutumia Mfumo wa Kijani Ilan Chatbot kikamilifu katika kupata majibu yote ya maswali kuhusu ilani na utekelezaji wake na kupata taarifa na kukuza uelewa.

“Twendeni tukatumie mfumo huo ili kuondoa upotoshaji unaofanywa na watu wasiokuwa na mapenzi mema na taifa letu kwa kuwaambia na kuwaonyesha watanzania Ukweli” ameongeza kawaida.
Awali Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM) Taifa Nl Halid Mwinyi amesema mfumo huo utawezesha mawasiliano ya moja kwa moja ambapo mtumiaji ataweza kuliza maswali na kupokea majibu kwa haraka na njia rahisi pamoja na kijifunza kuhusiana na uchaguzi na ilani ya CCM.

Ameongeza kuwa Mfumo utaleta mambo mbalimbali hususani kutoa taarifa kwa haraka, sahii naza kidigital kuhusu ilani ya ccm, miradi ya maendeleo na namna jamii inavyonufaika husani vijana.
“Kuwezesha vijana kuuliza maswali na majibu ya moja moja kwa kupitia mfumo huu wa kidigitali na kuongoza na kuwakumbusha vijana kuhusu nafasi yao katika maendeleo ya Taifa na ushiriki wa kisiasa, kukuza matumizi ya kitekonlojia kuhusu akili mnemba katika elimu ya siasa na utawala bora” amesema Mwinyi.
