TAJU YASISITIZA AMANI SIKU YA UCHAGUZI

Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam

TAASISI ya Tanzania Jumuishi  (TAJU) imewataka viongozi na wasimamizi wa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 kusimamia zoezi hilo kwa weledi  ili kila mshiriki aridhike  na mchakato huo na matokeo kwa ujumla kuepuka vurugu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam  lOktoba 25, 2025 katika kikao cha waru wenye ulemavu ukilichoratobiwa na TAJU,Katibu Mkuu wa taasisi hiyo  Innocent Siriwa alisema usimamizi wa uchaguzi wa haki na unaoridhisha utaimarisha amani  na kuwaponya wenye ulemavu.

“Tunajua fika kuwa wenzetu hampendi kuona watu wenye ulemavu wakitaabika na machafuko yanayoweza kuzuilika,tulio wengi ni mashahidi hapa tunapotembelea kambi za wakimbizi zilizopo hapa kwetu Tanzania hatujaona wakimbizi wenye aina yoyote ile ya ulemavu.

“Kila mmoja ajiulize je katika nchi hizo ambapo wakimbizi wanatoka hakuna watu wenye ulemavu,kama watu hao wapo je kwa nini  hawaonekani kwenye kambi za wakimbizi?Kwa mantiki hii watu wenye ulemavu wanahitaji amani zaidi kuliko kundi lolote lile  katika jamii,”alisema Siriwa.

Alisema pia washiriki wote wa uchaguzi kwa maana ya wagombea wa ngazi mbalimbali wa vyama vya siasa Waringstown sheria zilizopo kujiepusha na vitendo vya vurugu na uvunjifu wa sheria.

“TAJU ina uzoefu  kwakuwa imekuwa ikiona mara nyingi chaguzi zikigeuka  chanzo cha vurugu na uvunjifu wa amani katika mataifa mengi ulimwenguni,kwa nia nzuri tumeona tuoyoshe ghafla hii yakuombea uchaguzi mkuu ulio mbele yetu ili nchi yetu iendelee kuwa kisiwa cha amani na salama kwa kila Mtanzania wakiwemo  watu wenye ulemavu,”alisema Siriwa.

Aliongeza kwakuwaomba viongozi wa dini kwakuwasaidia sala,dua,maombi ili nchi iendelee kuwa amani na kuukabidhi uchaguzi mikononi mwa Mungu.

Naye Mwenyekiti wa TAJU Ngonge Ndonge alisema ni wakati wa Watanzania kutambua umuhimu wa amani ili kuweza kuwaokoa watu wenye ulemavu.

“Sisi walemavu huwa tunaonekana kama hatuathiriki endapo kunatokea machafuko lakini sisi ni waathirika wakubwa endapo amani haitakuwepo,*alisema Ndonge