Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam
MKUU wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amewataka wenyeviti wa wa serikali ya mtaa wa mkoa huo kuwa walinzi wa miundombinu ya umeme katika maeneo yao.
Akizungumza katika kikao kilicho wakutanisha WenyeViti wa serikali za mitaaa pamoja ma Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) jiji la Dar es Salaam kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Albert Chalamila, Mpogolo alisema kuwa kumekuwa na lawama nyingi na changamoto za hali ya upatikanaji wa umeme ikiwemo inayosababishwa na wizi wa miundombinu ya umeme pamoja na baadhi ya watu kujiunganishia umeme kiholela.

“Sisi kama WenyeViti wa SERIKALI za mitaaa tunaowajibu wakulinda Miundombinu ya SERIKALI kwakushirikiana na Tanesco kulinda Miundombinu,” alisema Mpogolo.
Mpogolo aliongeza kuwa ni vyema viongozi wa serikali za mitaa ikiwemo wenyeviti kushirikiana na shirika kulinda miundombinu hiyo
“Tanesco ni wakati wenu sasa kushuka hadi ngazi za mitaa ambapo wananchi wanapatikana ilikuweza kutatua changamoto za upatikanaji wa umeme,”alisema Mpogolo.
Amesisitiza kuwa wenyeviti wa ndio wanaowajua wananchi kwa ukaribu pamoja na changamoto zao ikiwemo ukosefu wa umeme.

Awali Mwakilishi Mkurugezi Mkuu wa Shirika la Tanesco, Irene Gowele alisema kuwa hali ya Upatikanaji wa Umeme Katika Mkoa wa Dar es Salaam na Wilaya zake umezidi kuimarika.
amesema azima ya Mkutano huo ni kukutana na wenyeviti wa serikali za mitaaa katika Mkoa wa Dar es Salaam ilikuweza kukuza mahusiano na shirika Hilo ,ili kuweza kutoa taarifa za Maendeleo ya Miradi ya Shirika la Tanesco katika Maeneo yao.
Amesema kuwa Azima ya mkutano huo,ni kuhakisha miundombinu ya umeme inalindwa.
“Lengo ni kuhakikisha Huduma za Upatikanaji wa umeme zinaimarika, sambamba na Miundombinu ya Umeme inalindwa,, Amesema Muwakilishi wa Mkurugezi wa Tanesco Irene Gowele.
Naye Mwenyekiti wa wenyeviti wa serikali mkoa wa Dar es Salaam Juma Mwengamno amesema Kwa Siku za hivi karibuni Huduma za Umeme zimeimarika Ambapo Hadi Sasa Jumla za Megawati MW 2,215 zitokanazo na Uzalishaji wa Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere zimeimarika kwa Matumizi ya Viwandani.


