TCB YASISITIZA KUENDELEA KUWA MDAU MKUBWA WA MAENDELEO VISIWANI ZANZIBAR

Na Mwandishi Wetu,Zanzibar

Benki ya Biashara Tanzania (TCB) imeungana na wananchi wa Kiziimkazi Zanzibar kwenye siku ya utalii kusherehekea ufahari wa utamaduni wa Kitanzania, vivutio vya utalii, umoja na mshikamano katika tamasha la Kizimkazi linaloendelea kufanyika visiwani Zanzibar.

 Benki hiyo imeendelea kusisitiza dhamira yake ya kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika vipaumbele vyake katika kukuza maendeleo ya kiuchumi, kutengeneza ajira, na kuwezesha ujumuishi katika kukuza uchumi wa buluu na upatikanaji wa huduma za kifedha visiwani humo.

Akizungumza wakati wa tamasha la Kizimkazi, Mkurugenzi  Mtendaji wa TCB Adam Mihayo amebainisha, dhamira ya Tcb ya  kukuza maendeleo ya kiuchumi na uchumi jumuishi ni dhahiri katika kila jambo wanalolifanya kwani wanaelewa kwamba mfumo thabiti wa kifedha ni uti wa mgongo wa uchumi imara. 

Mihayo amesema kaema sehemu ya dhamira hii, Benki ya TCB imejizatiti kutumia fursa mbalimbali lengo likiwa kuboresha maendeleo ya kiuchumi ya Wazanzibari na  Mojawapo ya mikakati hiyo ni mkataba wa makubaliano uliotiwa saini hivi karibuni baina ya benki na Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (ZEEA).

“Ushirikiano huu ni mpango wa utoaji wa mikopo inayolenga kuwanufaisha wanawake, vijana na makundi maalum wanaojihusisha na shughuli za kiuchumi visiwani Zanzibar Lengo  kuu ikiwa ni kuvifikia vikundi 70, na tayari TZS milioni 151 zimekwisha tolewa kati ya TZS milioni 300 zilizotengwa kwa ajili ya kuwainua wajasiriamali,” amesema Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TCB Adam Mihayo. 

Mihayo amebainisha kuwa mpango huo unakusudia kuchochea ukuaji wa biashara, ongezeko la ajira, na maendeleo ya kiuchumi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Mbali na mkakati huo, Benki ya TCB imejikita kuinua uchumi wa buluu hususani kilimo cha mwani. Ikitambua mchango mkubwa wa zao la mwani katika uchumi wa ndani, TCB imekusudia kuhakikisha kwamba wakulima hawa wanapata mikopo nafuu ili kufikia malengo yao.

 Kwa kuwawezesha kiuchumi, TCB pia inawasaidia kuboresha maisha yao na kuchangia katika ujenzi wa uchumi wa Zanzibar kwa ujumla.

Kupitia programu na ushirikiano mbalimbali, tunakusudia kuimarisha uchumi na kujenga mazingira imara na rafiki kwa wote na wanaposherekea tamasha hili la Kizimkazi, tunasherehekea pia kasi ya maendeleo ambayo kila mmoja ni mshiriki.

” Nitoe wito kwa wadau wenzangu tuendelee kushirikiana pamoja kujenga uchumi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.”amesema Mihayo.

Benki ya Biashara Tanzania imejipambanua kuendeleza lengo lake la kusaidia miradi mbalimbali inayochangia maendeleo na kujenga uchumi jumuishi kwa  kutoa bidhaa na huduma nafuu na kwa wote, benki inakuwa moja ya wadau muhimu katika mfumo wa uchumi wa taifa na maendeleo yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *