KIJIJI KWA KIJIJI DAWASA CHALINZE

Na Mwandishi Wetu,Chalinze

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeendelea na uelimishaji wa makundi mbalimbali ya kijamii juu ya utunzaji na uhifadhi wa Miundombinu ya maji.

Uelimishaji huo pia umejikita pia katika kuielekeza jamii matumizi sahihi ya huduma ya Majisafi pamoja na kusikiliza changamoto za kihuduma kwa Wananchi wanaohudumiwa na mamlaka.

Elimu hii imetolewa  kwa Wananchi wa Kijiji cha Manga kilichopo Wilaya ya Handeni , Mkoani Tanga ambao ni wanufaika na utekelezaji wa Mradi wa Maji Chalinze awamu ya tatu uliokamilika kwa asilimia 100.

Afisa Maendeleo ya Jamii DAWASA Elizabeth Eusebius ametumia nafasi hiyo kutoa ufafanuzi wa hatua mbali mbali zinazochukuliwa na Mamlaka katika kuimarisha huduma ya maji katika Kijiji hicho ikiwa ni pamoja na kufunga  pampu mpya za maji.

Amesema ufungaji wa pampu hizo mpya unaenda sambamba na kuimarisha mfumo wa umeme wa njia tatu katika tenki la  maji Tengwe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *