Na Aziza Masoud,Dar es Salaam
BENKI ya Equity imesema wafanyabiashara ambao wanatumia bidhaa za kampuni ya Said Salim Bakhresa(SSB) kwa sasa wana uwezo wakukopeshwa bidhaa hiyo hadi zaidi ya Sh Milioni 300.
Akizungumza wakati wa kusaini makubaliano hayo leo,Mkurugenzi wa biashara wa benki ya Equity Leah Ayoub amesema makubaliano hayo yaliyoanza 2021.
“Tunajua wasambazaji na wajasiriamali wengi wanapata ya mitaji na kupata changamoto ya ribatukaona tunarahisishe huduma zetu kwa wateja na wasambazaji wa Azam.
“Tumeingia makubaliano kati ya benki ya Equity na kampuni ya Bakhresa yenye lengo la kutoa mikopo kwa wafanyabiashara wa unga,mfanyabiashara atakuwa na iwezo wakukopa fedha kwa ajili ya kuoata bidhaa hiyo mpaka zaidi ya Shilingi Milioni 300,”amesema.
Amesema lengo ni kuhakikisha wafanyabiashara wanakuza mitaji ambapo kama benki wanatamani wateja hao wakope zaidi ya Sh Milioni 300.
Amesema mkopo huo hautakuwa na riba isipokuwa mteja atalipa kamisheni yakuanzia asilimia 0.5 mpaka 1.5 ambapo mkopaji atapaswa kulipa fedha hizo kuanzia siku saba hadi 30.
“Hii ni fursa ya kukuza mtaji wako kwa haraka,tumeamua kujitoa kwa wajasiriamali na kuwawezesha wapate huduma kwa urahisi bila vikwazo vingi ambapo mteja hata kama hana akaunto ya Equity ana uwezo wakuifungua kiganjanjani mwake akapata mkopo,”amesema Leah.
Naye Mkurugenzi wa Uhusiano wa kampuni Bakhresa Group Hussein Sufiani amesema makubalino haya yatamsaidia mteja ambapo badala kuhangaika kutafuta mfadhili au mdhamini wakumpatia fedja anaweza kwenda benki au kutumia mtandao kupata huduma.
“Hii nayo ni kidigitali,utapata huduma hiyo kwa mfumo wa sms (ujumbe mfupi),sio lazima uende benki kufanya transfer (kuhamisha) inafanyika moja kwa moja ukishafanya oda yako,kadri unavyozidi kukopa kiwango kinakua,”amesema Sufiani.
Amesema huduma hiyo itawasaidia zaidi wateja wao hasa wadogo hivyo amewahimiza kuchangamkia fursa hiyo.