Na Aziza Masoud,Dar es Salaam
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Abdalla Ulega amewataka watafiti kushirikiana na wizara na taasisi mbalimbali pindi wanapohitaji kutoa matokeo ya tafiti zao ili kupunguza taharuki zinazotokea katika jamii pindi wanapotoa matokeo yao.
Ulega alitoa ushauri huo wakati akifungua jukwaa la tasnia la kuku na ndege wafugwao ambapo alieleza kuwa hivi karibuni kulikuwa taarifa ya utafiti kuhusu wasiwasi wa ulishaji kuku huku ikidaiwa kuwa na madawa ambayo yanatumika kukuza kuku hao jambo ambalo lilizua taharuki.
“Natoa wito kwa watafiti kushirikiana na wizara ya mifugo wanapofanya tafiti zao ili kuepusha taharuki,hivi karibuni tulipata taarifa za kiutafiti walikuja kusema juu ya wasiwasi wao kuhusu ulishaji wa kuku,hii ilizua taharuki hivyo ni vizuri tuwe tunawasiliana na tunapofanya tafiti kama hizi,”alisema Ulega.
Alisema serikali inawaheshimu na kuwathamini watafiti kwakuwa lakini wanatamani wanapofanya tafiti kabla yakuzipeleka kwa walaji kuwe na mkakati wa pamoja wa jinsi yakuwasilisha taarifa kwa jamii.
Alisema tafiti ya namna ya namna kuleta taharuki na kusababisha watu kutokula nyama hivyo kuisababishia jamii kuwa na upungufu wa protini.
Amesema asilimia 55 ya kaya Tanzania zinafanya ufugaji kwakuwa mifugo haiitaji eneo kubwa.
“Kwa mujibu wa taarifa ifikapo 2030 nyama ya kuku itakuwa na uwezo wakuzalisha protini kwa asilimia 41 ya protini itakanayo na wanyama,”alisema Ulega.
Alisema kutokana na umuhimu wa sekta ya kuku katika kufanikisha usalama wa chakula na ukuaji wa uchumi nchini dhamira ya serikali ni kuunga mkono sekta hiiyo kupitia miradi inayolenga vijana, ubunifu, na uendelevu.
Naye Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Shirika la Uboreshaji wa Kijana Tanzania (AGRA) Vianey Rweyendela alisema lengo la majukwaa kama hayo ni kuhakikisha mkulima anaongeza tija.
“Tija ni ushindani wakulima ukiwauliza kuhusu bidhaa zai wanasema bei ni ndogo sokoni bei haiwezi kuwa ndogo,lazima mkulima aongeze tija alafu anakuwa mshindani sokoni,”alisema.
Alisema katika jitihada zote hizi mdau wa kwanza ni serikali ambaye anatakiwa kumwekezesha mkulima pembejeo na kumsaidia mkulima katika masoko.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Inayojihusisha na Kukuza Kilimo Upande was Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) Geofrey Kirenga
Geoffrey Kirenga alitoa ujumbe wa kuhamasisha akitumia mfano wa Chips Mayai ili kuonyesha umuhimu wa kiutamaduni na kiuchumi wa bidhaa za kuku nchini Tanzania.
Alisema, “Kuku ni chanzo muhimu cha lishe na kipato kwa maelfu ya familia. Tunapaswa kuendelea kuimarisha sekta hii kupitia ubunifu na uwekezaji.”