WANANCHI WATAKIWA KUWA NA UTAMADUNI WA KUTENGANISHA TAKA

Na Aziza Masoud,Dar es Salaam

JAMII imetakiwa kuwa na utamaduni wa kutenganisha taka rejeshi  na taka ambazo sio rejeshi ili kuweza kupunguza uzalishaji wa taka ambapo kwa sasa  jiji la Dar es Salaam linazalisha  tani 1320 kwa siku. 

Akizungumza wakati wa kuzindua mradi wa taka  sifuri ‘zero waste’ katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Jangwani unaosimamiwa  na shirika la Mazingira Plus,Mkuu wa Kitengo cha Uhifadhi wa Taka na Usafi wa Mazingira cha  jiji la Dar es Salaam,Philipo Beno amesema  mradi wa taka sifuri kama utaweza kuwafikia wananchi wa kawaida utakuwa msaada mkubwa wakupungza uzalishani wa taka ambazo zinaenda  dampo. 

“Halmashauri ya jiji la Ilala kwa siku wanazalisha tani 1320 za taka hiyo ni kwa siku,taka hizi zote zinatakiwa zitolewe na  kupelekwa dampo,tukikaa vizuri na zero waste suala hili likashuka chini kwa jamii  tukafanya utaratibu wakutenganisha taka ambapo kufanya hivyo  dampo litachukua taka chache,”amesema Beno. 

Amesema kwa upende wa halmashauri wamefanikiwa katika suala la utenganishaji taka rejeshi na zisizo rejeshi hospitalini ambapo wana utaratibu mzuri wa ukusanyaji taka. 

Amesema kwakuweka mradi wa taka ziro shuleni utasaidia  kwakiasi kikubwa kwa wanafunzi na walimu ambapo elimu hiyo wataipeleka katika jamii na kuanza kutenganisha taka. 

“Mradi huu wa zero waste  kwanza kwetu ni msaada mkubwa kwa sababu tunaenda kupunguza kiasi cha taka ambazo tunaenda kuzitupa dampo na kufanya madampo yetu yakae muda mrefu. 

“Pia mradi huu kwakutumia vijana tunategemea jamii ambayo itaenda kubadilika katika utunzaji wa taka pia kupitia taka hizi tutafadika kwakupata mbolea mbalimbali,”amesema Beno. 

Naye Mkuu wa Kitengo cha Mazingira,Mazingira Plus Ramadhani  Mwakae  amesema mradi wa taka sifuri uliokabidhiwa shule ya sekondari Jangwani ni hatua ya pili ambapo hatua ya kwanza walianza shule ya sekondari  Kibasila  iliyopo wilaya ya Temeke. 

Amesema kupitia mradi huo shule hiyo imejengewa kizimba chenye vyba sita ambavyo vinatenganisha aina mbalimbali za taka ambapo wanafunzi pia wanekuwa na uwezo wakutengeneza  bustani za mboga mboga ba kutumia mbolea zitokanazo na taka mbalimbali.

“Dhumuni la mradi huu ni kupambana na mabadiliko ya tabia nchi hususani kudhibiti  uchafuzi wa taka mashuleni lakini,pia malengo ya mradi huu ni kufanya uchechemuzi wa sera na kuishauri serikali juu ya mpango mzima wa kutokomeza  sera zakukabiliana au kudhibiti uchafunzi wa taka katika shule zetu,”amesema  Mwakae.

Amesema mbali na Jangwani mradi huo pia wataupeleka  katika shule za Dar es Salaam Sekondari ambao utafanyika katika wilaya ya Ilala. 

“Tutafanya pia katika shule za msingi ambayo itafanyika katika shule ya Temeke,niwasihi wadau mbalimbali ikiwemo taasisi tunnganie katika kupambana na mabadiliko ya tabia nchi lakini pia kutoa elimu jumuishi ya mazingira,”amesema Mwakae

Amesema takwimu zinaonyesha tatizo kubwa la mabadiliko ya tabia nchi ni tatizo la mazingira hasa plastiki na taka ozo hivyo tunatasihi  mashirika yasiyokuwa na serikali tuingie  katika kampeni hii ili ifikapo  2030 jamii itengeneze  mtandao wa taka sifuri. 

“Tutengeneze  taka sifuri sio shuleni tu hadi majumbani,kwa na taka amabazo asilimia 80 ya taka zinazozalishwa zirudi kwenye matumizi mengine kwakuwa kwa sasa kila mtu anahisi kuwa anawajibika na uchafuzi wa mazingira,suala la mazingira ni suala mtambuka,”amesema Mwakae

Kwa upande wa Dorothee Braun ambaye ni  Mwakilishi wa Taasisi ya Kimataifa ya Nagu iliyopo nchini Ujerumani ambayo inahusika na Mazingira na Mabadiliko ya Hali ya Hewa amesema wao kama wafadhili wanaipongeza taasisi ya mazigira plus kwakuchukua hatua  kubwa yakuelelimisha wanafunzi kuhusu taka rejeshi.

“Duniani kote  taka rejeshi  ni tatizo  kubwa hata sisi Ulaya tulianza kwakuweka utaratibu wa kutenganisha taka,ni jukumu letu kuwasapoti watu wa hapa kuelimisha na kutafuta njia nzuri kwao kutafuta suluhisho la taka rejeshi,” Braun.

Amesema walianza   kushirikiana na Mazingira Plus  mwaka jana kupitia mradi wa shule ya Sekondari Kibasila ambao waliufanya kwa mafanikio. 

“Katika miradi hii shule moja inagharimu EURO 5000 mpaka 7000  sisi tunataka waendelee  kwa sasa tunataka kuendelea katika shule zote hivyo mradi utachukua muda lakini pia waende  kijijini kwakuwa wanachafua mazingira na kuathiri  kilimo,”amesema Braun.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *