ASILIMIA 94.84 WAJIANDIKISHA KUPIGA KURA SERIKALI ZA MITAA

Na Aziza Masoud,Dar es Salaam

JUMLA ya wapiga kura 31,282,331 sawa na asilimia 94.83  ya lengo  waliopaswa kuandikishwa katika daftari la wapiga  kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu ambapo matarajio ilikuwa kuandikisha watu 32,987,579 .

Takwimu hizo zimetolewa leo na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamedi Mchengerwa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake jijini Dar es Salaam.

Amesema zoezi hilo ambalo lilifanyika kwa siku kumi kuanzia Oktoba 11 mpaka Oktoba 20 ambapo mikoa yote 26 imefanya kazi nzuri katika zoezi hilo la uandikishaji. 

“Jumla ya wapiga kura 31,282,331 wamejiandikisha kupiga kura sawa na asilimia 94.83 ya lengo la kuandikisha watu 32,987,579 ambapo wanaume ni 15,236,772 sawa na asilimia 48.71 na wanawake ni 16,045,559 sawa na asilimia 51.29,”amesema Mchengerwa.

Amesema matokeo hayo yanaonesha kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya wananchi waliojitokeza kujiandikisha ikilinganishwa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2019 ambapo waliandikishwa wapiga kura 19,681,259 sawa na asilimia 86 ya lengo lililokuwa limewekwa la kuandikisha wapiga kura 22,916,412. 

“Jumla ya wapiga kura 31,282,331 wamejiandikisha kupiga kura sawa na asilimia 94.83 ya lengo la kuandikisha watu 32,987,579 ambapo wanaume ni 15,236,772 sawa na asilimia 48.71 na wanawake ni 16,045,559 sawa na asilimia 51.29,”amesema Mchengerwa.

Akifafanua mwenendo wa uandikishaji wa wapiga kura ndano ya siku kumi  ambapo ulikadiriwa kuandikishwa asilimia kumi kwa siku ili kufikia lengo lililokusudiwa.

Amesema siku ya kwanza waliandikishwa watu 3,882,994 sawa na asilimia 11.82 ya lengo la siku la kuandikisha kwa asilimia 10 huku Slsiku ya pili waliandikishwa watu 2,554,375 sawa na asilimia 7.78 ya lengo la siku.

“Siku ya tatu waliandikishwa watu 2,660,084 sawa na asilimia 8.10,siku ya nne waliandikishwa watu 2,544,844 sawa na asilimia 7.75,siki ya tano waliandikishwa watu 2,460,664 sawa na asilimia 7.46.

“Siku ya sita waliandikishwa watu 2,472,605 sawa na asilimia 7.50,siku ya saba waliandikishwa watu 2,971,219 sawa na asilimia 9.01,siku ya nane waliandikishwa watu 3,409,211 sawa na asilimia 10.33,”amesema Mchengerwa.

Amesema siku ya tisa waliandikishwa watu 3,813,999 sawa na asilimia 11.56 ,siku ya kumi waliandikishwa watu 4,512,336 sawa na asilimia 13.68 ya lengo la siku.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *