BANDARI YA TANGA INAVYOWEZESHA UTELEKEZAJI WA MIRADI YA KIMKAKATI HUKU MIZIGO IKIONGEZEKA

Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kupitia Bandari ya Tanga, inachukua nafasi muhimu katikakuwezesha miradi mikubwa ya kimkakati kitaifa na kikanda, ikiwemo mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) lenye urefu wa kilomita 1,443. 

Bomba hili litahudumia usafirishaji wa mapipa 216,000 yamafuta ghafi kwa siku kutoka Hoima, Uganda, hadiChongoleani, Tanga, Tanzania.

Ingawa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ndilo linalosimamia mradi huo, Bandari ya Tanga inatoamsaada muhimu, kwa mujibu wa Meneja wa Bandari ya Tanga Masoud Mrisha.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara yaeneo la bandari wiki hii, Mrisha alisema bandari hiyoimekabidhi eneo la ekari 75 Chongoleani kwa TPDC kwa ajiliya mradi wa EACOP.

“Kwa kukabidhi ekari 75, ambazo niasilimia 36.2 ya eneo letu la Chongoleani, tunaonyesha nikiasi gani tunathamini mradi huu wa kimkakati kwa taifa na kanda,” amesema.

Mrisha ameeleza kuwa bandari pia imepanga eneo la mitaza mraba 2,842 katika Gati la 2 ili kuwezesha upokeaji na upakiaji wa haraka wa vifaa vya ujenzi wa bomba hilo. “Meli zinazobeba vifaa vya mradi wa EACOP zinapowasili, zinapakuliwa na kupakiwa mara moja,” aliongeza.

Mbali na msaada wa kiufundi, Bandari ya Tanga inatoamafunzo kwa wafanyakazi wa EACOP kuhusu jinsi yakukabiliana na hali ya kuvuja kwa mafuta na changamotozingine za baharini. Hatua hizi ni sehemu ya jukumu la bandari katika kukuza maendeleo ya kikanda kupitia miradimikubwa kama EACOP.

Bandari ya Tanga, ambayo imepata maboresho makubwakatika miaka ya hivi karibuni, inaendelea kujidhihirisha kamakitovu muhimu katika ukuaji wa miundombinu ya kikanda, ikiwa ni sehemu ya mipango ya kiuchumi ya Tanzania. 

Serikali imewekeza Sh429.1 bilioni katika kuboresha Miundombinu na uwezo wa Bandari ya Tanga katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Mrisha amesema kuwa uwekezaji huo umeiwezesha bandari hiyo kuhudumia melikubwa zaidi na kuongeza uwezo wa kupitisha mizigo, hatuainayothibitisha umuhimu wake kama kituo kikuu cha baharinikikanda.

Bandari ya Tanga ilijengwa mwaka 1914 kwa ajili yakuhudumia mahitaji ya kibiashara na kilimo ya kaskazini mwa Tanzania.

Hivi sasa, bandari hiyo imeboreshwa na ina uwezowa kuhudumia meli kubwa zaidi kuliko hapo awali. Maboresho hayo, ambayo yalifanyika katika awamu mbili, yalihusisha kuongeza kina cha maji kutoka mita 3 hadi mita13 na kupanua njia ya kugeuza meli.

Aidha, sehemu yauwekezaji huo wa Sh429.1 bilioni ulitumika kununua vifaa vipya vya kushughulikia mizigo na kupanua gati mbili hadi kufikia upana wa mita 450. Kwa maboresho haya, meli sasa ainaweza kutia nanga moja kwa moja bandarini, tofauti na awali ambapo meli zilipaswa kusimama umbali wa kilomita1.7 kutoka bandari na kupakuliwa kwa kutumia mabaji. 

Maboresho haya yameondoa gharama ya $1.3 kwa tani moja ya mizigo iliyokuwa ikitozwa na TPA kwa mizigoiliyosafirishwa kupitia mabaji.
“Sasa, hata meli kubwazinaweza kutia nanga moja kwa moja katika Bandari yaTanga, na hivyo kurahisisha shughuli zetu,” alieleza Mrisha.

Maboresho hayo pia yameongeza uzalishaji wa Bandari yaTanga. Meli kubwa ambazo hapo awali zilihitaji zaidi ya siku tano kupakuliwa sasa zinapakuliwa ndani ya siku mbili tu.Katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa sasa, bandari hiyo ilishughulikia tani 333,643 za mizigo, ikipita lengo lake la tani 283,225 kwa asilimia 17.

Hii ni ongezeko kubwaikilinganishwa na tani 204,000 zilizoshughulikiwa katikakipindi kama hicho cha mwaka wa fedha wa 2023/24.

Katika mwaka mzima wa fedha wa 2023/24, Bandari yaTanga ilishughulikia tani 1,191,480 za mizigo, ikilinganishwana tani 890,901 mwaka uliopita. Aidha, bandari hiyoilihudumia meli 113 katika robo ya kwanza pekee, ikizidi kwambali lengo la kuhudumia meli tano.

Uwezo ulioboreshwa wa bandari umeiwezesha kuanzakushughulikia bidhaa ambazo awali hazikuwezakushughulikiwa, kama vile salfa, shaba, na nitrati za amonia. Bandari ya Tanga pia imeanza kupokea meli zinazosafirishamagari, hatua inayopanua wigo wa shughuli zake.

Miongoni mwa maboresho muhimu ni ununuzi wa vifaa vipyavya kushughulikia mizigo, ikiwemo kreni mbili za bandari zenye uwezo wa tani 100 kila moja, kreni ya magurudumu ya Rubber Tyred Gantry, Empty Handler, na Grab yenye uwezowa tani 15. Vifaa vingine ni pamoja na vihamishi (forklift) sita vyenye uwezo tofauti na vinyanyua vitatu vya makontena, viwili kwa ajili ya makontena ya futi 40 na kimoja cha futi 20.

Maboresho haya yanatarajiwa kuongeza zaidi uwezo na ufanisi wa Bandari ya Tanga katika kushughulikia mizigo Bandarini, na kuchangia ukuaji wa biashara za kikanda na uchumi wa Tanzania kwa ujumla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *