GCLA KUANZA KUKAGUA RANGI ZENYE MADINI RISASI

Na Aziza Masoud,Dar Es Salaam

MAMLKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA)  imesema  wanaanza utaratibu wakukagua rangi za nyumba  lengo ni kubaini uwepo wa madini ya risasi  katika rangi zinazotengenezwa ndani na nje ya nchi.

Akizungumza wakati wa mkutano uliowakutanisha wadau wa rangi ikiwa ni sehemu  kuazimisha wiki ya kuzuia matumizi ya sumu itokanayo na madini ya risasi,Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti GCLA ,Daniel Ndiyo amesema kwa mujibu wa Shirika la Afya Dunia (WHO)  madini hayo ambayo yanapatikana zaidi katika rangi za nyumba yamebainika kuwa na athari kubwa katika mwili wa binadamu.

“Kila mzigo utakaoungizwa kutoka nje ya nchi wa rangi  ili kulinda umma wa watanzania tutakuwa tunachukua sampuli tutapima kujiridhisha kwamba uko salama na madini ya risasi.

“Hatua ya pili itafanyika kwa wauzaji  tunachukua sampuli na kupima,tutaendelea kufanya ufuatiliaji tunaweza kufika kwenye kiwanda chako tunaangalia au mzigo ukija tunaangalia ,sisi ni wadhibiti wenu hatutaki tuwe wadhibiti tunataka kuwa wawezeshaji kwenye hili naomba tufanye kazi pamoja lengo lakufanya ili ni kulinda nchi yetu,”alisema Ndiyo.

Amesema zoezi hilo ni muhimu ili kuokoa umma wa watanzania kwakuwa rangi  imekuwa ikitumika kupaka kwenye mabati ambapo watu katika kipindi cha mvua  hutumia maji hayo ikiwa uhakika wa usalama wake kwa matumizi haujulikani.

Alisema ikiwa kama sehemu yakuanza kuwalinda watanzania walifanya utafiti mdogo kuhusu madini ya risasi kwenye kwakuchumua kampuni kumi za rangi kwakuchukua sampuli 31 za rangi humu sampuli  nzima zikiwa 29 na sampuli mbili zilibainika kuwa  kasoro ambayo ni sawa na asilimia 6.4.

Aidha ametoa rai kwa wadau wanaohusika kwenye tasnia ya rangi,kuondokana na dhana potofu ambayo imezoeleka,kutumia  maziwa pekee kwa ajili ya kudhibiti sumu mwilini kwani inaweza kudhibiti baadhi ya sumu chache pekee  na sio zote  kama ilivyozoeleka.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaalam ya Kituo cha Taifa cha Kudhibiti Matukio ya Sumu Profesa Amos Mwakigonja amewaagiza watu wanaoshughulika na kazi zinazohusiana na madini ya risasi  kuunga juhudi zinazofanyika kwakuachana na shughuli ambazo zinahusiana na usambazaji wa madini hayo katika mazingira,ambapo itasaidia kuepusha madhara kwa watu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *