WATAHINIWA 974,229 WAFAULU DARASA LA SABA

Na Aziza Masoud,Dar es Salaam

BARAZA la Mtihani la Tanzania (NECTA) limesema jumla ya  watahiniwa 974,229 sawa na asilimia 80.87  kati ya watahiniwa 1,204,899 ambao asilimia ni 97.90  ya waliofanya mtihani wakumaliza elimu ya msingi 2024  wamefaulu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Oktoba 29,Katibu Mtendaji wa NECTA Dk.Saidi Mohamed amesema jumla ya watahiniwa 1,230,774 walisajiliwa kufanya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi ambapo kati ya hao wasichana 666,597 (54.16%) na wavulana 564,177 (45.84%). 

Amesema kati ya watahiniwa waliosajiliwa, watahiniwa wenye mahitaji maalum walikuwa 4,583 sawa na asilimia 0.37.

“Kati ya watahiniwa 1,230,774 waliosajiliwa, watahiniwa 1,204,899 sawa na asilimia 97.90 walifanya mtihani wakiwemo wasichana 656,160 (98.43%) na Wavulana 548,739 (97.26%). 

“Jumla ya watahiniwa 974,229 sawa na asilimia 80.87 ya watahiniwa wenye matokeo wamefaulu Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi 2024.,”amesema Dk.Mohamed.

Amesema mwaka 2023 watahiniwa waliofaulu walikuwa asilimia 80.58 hivyo ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 0.29. 

“Kati ya watahiniwa 974,229 waliofaulu,wavulana ni 449,057 sawa na asilimia 81.85 na wasichana ni 525,172 sawa na asilimia 80.05. 

“Mwaka 2023 wasichana waliofaulu walikuwa asilimia 80.58 na wavulana waliofaulu walikuwa asilimia 80.59,hivyo , ufaulu wa wasichana umeshuka kwa asilimia 0.53 na ufaulu wa Wavulana umeongezeka kwa asilimia 1.26.,”amesema.

Alisema ubora  wa ufaulu kwa watahiniwa waliopata madaraja ya A na B umeimarika ambapo watahiniwa 431,689 sawa na asilimia 35.83 wamepata madaraja ya A na Bikiwa ni ongezeko la asilimia 8.65 ikilinganishwa na mwaka 2023. 

Amesema kati ya watahiniwa 431,689 waliopata ubora wa ufaulu katika madaraja ya A na B, Wasichana ni 216,568 (33.01%) wakiwa na ongezeko la asilimia 9.09 na Wavulana ni 215,121 (39.21%) wakiwa na ongezeko la asilimia 8.28 ikilinganishwa na mwaka 2023.

Amesema  watahiniwa  25,875 (2.10%) hawakufanya Mtihani, kati yao wavulana ni 15,438 (2.74%) na wasichana ni 10,437 (1.57%).

Mwisho

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *