TRC:TRENI YA MCHONGOKO TUNAHUJUMIWA 

Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam

SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limesema tukio lililotokea Novemba  3,2024  ambalo lilisababisha  treni ya mchongoko (EMU)  kusimama kwa takribani saa sita  ni hujuma zilizohusisha kukatika ama kukatwa kwa nyaya (catenary) zinazochukua umeme kutoka njia ya umeme kupeleka kwenye treni.

Taarifa iliyotolewa leo Novemba 06,2024 na Mkuu wa Kitemgo cha Uhusiano TRC,Fredy Mwanjala imesema taarifa zilizosambaa  kuwa treni hiyo ilizimika kutokana na changamoto za umeme si kweli kwakuwa hakuna treni ya mchongoko iliyopata hitilafu ya kiufundi.

“Tayari baadhi ya wahusika wamekamatwa na hatua stahiki dhidi yao zimeshaanza kuchukuliwa ikiwemo kufikishwa kwenye vyombo husika,tunawashukuru  wenzetu wa TANESCO kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa,shirika  linauhakikishia umma kuwa hakuna treni ya  iliyopata hitilafu ya kiufundi,”amesema Mwanjala.

Amesema TRC imeutaka umma  kupuuza taarifa potofu zinazosambazwa na watu mbalimbali na kwamba ukweli ni kwamba tangu kuanza kwa safari ya kwanza ya treni zinazotumia nishati ya umeme Juni 14, 2024 hakujawahi kuwa na changamoto ya umeme.

“Shirika linawakumbusha wananchi kuwa bado tuko kwenye kipindi cha mwaka mmoja cha matazamio, na kama changomoto zozote zinajitokeza, TRC itaujulisha umma kwa uwazi kama siku zote tunavyofanya, na taarifa rasmi mtazipata kwenye vyanzo vyetu rasmi na si vinginevyo.,”amesema Mwanjala.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *