Na Aziza Masoud,Dar es Salaam
MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA) imewataka wananchi wanaohitaji kuhudumiwa masuala mbalimbali yakikodi ikiwemo namba ya utambulisho wa biashara (TIN) kufika katika viwanja vya Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) maarufu kama Sabasaba kuweza kupata huduma hiyo
Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 30, 2025 Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipa Kodi na Mawasiliano wa TRA,Richard Kayombo alisema wameshiriki katika Maonesho hayo ya 49 kwa ajili yakuendeleza kutoa elimu ya kodi kwa wadau wanaofika katika viwanja hivyo.

“Tumeona tuje ili kuwaelimisha wadau mambo.mapya na ya zamani kama kuhusu Chuo chetu cha kodi,vivutio vya kodi,sekta za kilimo pia ukija bandana kwetu utapata huduma ya kupata TIN namba hapa hapa bandani,I”alisema Kayombo.
Alisema katika maonesho hayo mamlaka ina mambo mengi ikiwemo kuwaelekeza watu kuagiza bidhaa,kuwaelekeza bidhaa zenye misamaha ya kodi.

Alisema watembeleaji pia wataelekezwa jinsi ya kutoa taarifa kwa wafanyakazi wasio na maadili ili waweze kuchukuliwa hatua.
“Wateja pia tutawaelewesha jinsi ya kuwaripoi wafanyakazi ambao hawana maadili na tunawaelimisha tunachukua hatua gani kwa watu hao ili waweze kufanya kazi kwa maadili,”alisema Kayombo.
Alisema katika banda hilo kuna huduma za stampu za kodi kwa wateja na elimu ya a kupata elimu bidhaa zipi zinatakiwa kuwekwa stempu.

Alisema katika banda hilo pia kuna watalaam wakuelewesha kuhusu bidhaa bandia ambapo wateja watapata elimu hiyo kwa upana.
