GCLA YAWAITA WAJASIRIAMALI WANAOHUSIKA NA KEMIKALI KUJISAJILI SABASABA

MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GGLA) imewataka wajasiriamali wanaojishughulisha na kemikali kufika katika Maonesho ya 49 ya  Kimataifa Biashara Dar es Salaam (DITF) ili kuweza kupata elimu kuhusu kemikali pamoja na kufanya usajili wa bidhaa hiyo

Akizungumza Julai 5, 2025 katika viwanja vya maonesho ya Sabasaba Mkurugenzi wa Huduma za Uchunguzi wa Bidhaa na Mazingira Dk.Peter Shimo alisema mamlaka hiyo ipo katika maonesho hayo kwa ajili yakuendelea kutoa elimu ya masuala mbalimbali hasa ya katika masuala ya kemikali.

“Huduma tunazozitoa hapa ni pamoja na  za usajili wa kemikali,wahusika wanaofika hapa pia wanapata elimu kuhusu shughuli zetu pia tunasajili wajasiriamali wanaojihusisha na masuala ya  kemikali,”alisema Dk.Shimo.

Alisema wajasiriamali watakaotembelea banda hilo anbao wanajishughilisha na shughuli za kemikali bila usajili pia watapewa maelekezo ya taratibu zakufuata ili kukamilisha usajili.

Alisema mamlaka pia ina mfumo wa kusajili wajasiriamali mtandaoni kwa ajili ya watu ambao wapo mbali na watoa huduma hiyo.

 “Ambao wapo mbali  na ofisi zetu nao waje hapa kwenye banda ili wapate usajili kwa njia ya mtandao,”alisema.

Alisema  lengo la GCLA ni kuhakikisha jamii inapata elimu ya kemikali na mambo mengine yanayohusiana na mamlaka  katika maeneo yote.