Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limesema kuwa uchunguzi walioufanya wamebaini kuwa watanzania wanahitaji huduma bora za intaneti lakini za bei nafuu na kuahidi kuendelea kuboresha huduma zao kulingana na uhitaji.
Akizungumza wakati wa kuzindua kifurushi kipya cha T-Fiber,Meneja wa Promosheni wa TTCL Janeth Maeda,alisema wameendelea kusikiliza maoni,mahitaji, na matarajio ya Watanzania kutoka kila pembe ya nchi ili kuboresha huduma wanazozitoa.
” Tumejifunza kwamba, wananchi wanahitaji huduma rahisi kutumia, za gharama nafuu, lakini zenye ubora wa juu itakayotoa tafsiri ya thamani halisi kwa fedha wanazotumia katika hurakati za kuboresha maisha yao,”alisema Maeda.

Alisema kwa kutambua hilo, jana wanajivunia kuzindua rasmi huduma mpya iitwayo T. Fiber kidijitali.
“Triple Hub ni kifurushi kipya ambacho kimebuniwa kwa kuzingatia mahitaji ya kizazi cha sasa,kifurushi hiki kinajumuisha huduma tatu muhim yaani mfumo wa kifurushi kimoja, Bili moja, huduma tatu ambazo ni Intaneti (Unlimited Internet) kwa matumizi ya familia, ofisi, biashara, na hata mifumo ya kidigitali.

“Huduma ya Simu ya Mezani (Landline Voice Service) inayompa mteja fursa ya kupiga na kupokea simu kwa urahisi kupitia miundombinu ya faiba na ya tatu ni huduma ya intaneti na dakika kwa simu ya mkononi (Mobile Services),”alisema Maeda.
Alisema huduma hiyo itamwezesha mteja kupata vifurushi vyenye GB na Dakika za kutosha ambavyo vinaweza kutumika popote pale mteja alipo akiwa na Laini ya simu ya TTCL, na anaweza kuwaunganisha ndug na jamaa au wafanyakazi wake na kufurahia kasi ile ile.

Alisema hicho mimeundwa ili kurahisisha maisha, kupunguza gharama, na kutoa thamani kubwa zaidi kwa wateja wa kampuni hiyo.
Alisema TTCL inafungua ukurasa mpya wa kidijitali chini, Shirika la kwanza Tanzania la mawasiliano kutoa kifurushi kinachojumuisha huduma tatu kwa kwa pamoja lengo likiwa ni kuunganisha Watanzania wote kwa njia bora, rahisi na ya kisasa kwa gharama nafuu.
Alisema kifurushi kitakuwa kinapatikana kwa gharama nafuu ya Sh 70,000 kwa mwezi.


