’T-CAFE’ za TTCL kufungwa mtandao wa intaneti kwa bei nafuu

Na Aziza Masoud,Dar es Salaam

SHIRIKA ya Mawasiliano Tanzania (TTCL) imekuja na huduma mpya ambayo itahusisha kufunga mtandao  kwa bei nafuu katika maeneo yenye mkusanyiko wa watu kama vituo vya treni,viwanja vya ndege na mabasi inayojulikana kama(T-CAFE).

Akizungumza leo Julai 3, katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa(Sabasaba) Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL Zuhura Muro alisema  kampuni hiyo imekuja na huduma hiyo ambapo katika maeneo hayo ya mkusanyiko wa watu huku unapata mawasiliano ya mtandao pia  kutakuwa na huduma ya chai,vitafunwa pamoja na huduma nyingine.

‘Tumekuja ni kitu kingine cha Public WIFI  ambazo tunapeleka katika vyuo, maeneo yenye mkusanyiko wa watu,tumekuja na bidhaa mpya inaitwa T-CAFE wakati unaenjoy WIFI unapata huduma ya chai, vitafunwa na huduma nyingine,hii pia itasaidia kuileta  jamii pamoja na  kuchangamana na kuzungumza katika vituo hivyo,

‘Tunataka kupeleka katika sehemu mbalimbali, mfano katika vituo vya reli, ndege, mabasi ambapo tutaungana na wafanyabiashara ambao wana uwezo wa kutoa huduma za vinywaji na vitafunwa ili kuweza kuhakikisha kwamba watu wanaielewa T-CAFE inavyotoa huduma zake,’amesema Muro.

Amesema wamejipanga vizuri katika huduma hiyoi hivyo wanategemea kufungua milango zaidi ya kudigitali kuwezesha biashara.

Akizungumzia kuhusu ushiriki wao katikamaonesho hayo amesema ushiriki wao unaenda sambamba  na kauli mbiu inayosema ‘Tanzania ni mahali sahihi kwa biashara na uwekezaji’ na kwamba kama kampuni wana wajibu mkubwa kufanya biashara kama kampuni.

‘Rais Samia(Samia Suluhu Hassani) ambaye amefungua milango mingi na kuiweka Tanzania katika nafasi nzuri ya kuvutia uwekezaji,TTCL tuna wajibu mkubwa sana kwasababu katika karne hii  hakuna biashara iliyosimama kama hauna maunganisho ya kidigitali,’amesema Muro.

 Amesema kutokana na hali hiyo TTCL inafungua milango ya kidigitali kwa Tanzania nan chi zinazozunguka Dunia nzima.

‘Kutokana na kauli mbiu hii basi sisi tumejipanga kama shirika katika mikakati ambayo itawezesha wanaowekeza Tanzania kutoka nje na ndani ya nchi kuweza kuungana na dunia kidijitali uwe mahali popote unaweza kuunganishwa kidijitali kutokana na nguvu ya mawasiliano tuliyonayo,

‘Sisi ndo tumebeba dhamana ya kuendesha mkongo wa mawasiliano wa Taifa na tumejipanga vizuri katika mkakati mkubwa ambayo ni kuunganisha hizi biashara katika kila sehemu na mkongo unapelekwa katika tarafa zote za Tanzania,kutokana na kupelekwa kwa tarafa zote ina maana tunaunganisha mashirika yote ya kiserikali, umma, sekta binafsi katika mkongo, tuna data center ambayo tunawaunganisha watu na kuwawekea data zao ,’amesema Muro.

Amesema wanategemea pia TTCL kuwa  kitovu maalum cha malipo jamii yote ambapo yatakuwa yanapita TTCL na kuunganisha watu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *