‘Msiwafiche  watu wenye ulemavu’

Na Aziza Masoud,Dar es Salaam 

Riziki Ndumba ambaye ni fundi cherehani na mlemavu wa mikono amewataka wazazi wenye watoto wenye ulemavu kutowaficha badala yake wawatafutie shule wapate ujuzi.

Ndumba ambaye ni muhitimu kutoka Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA) Songea amesema tangu ahitimu mwaka 2021,alisema endapo wazazi wake na yeye wangemficha asingepata ujuzi hivyo angekuwa akiishi kinyonge kwakigezo cha ulemavu.

“Mimi naishukuru  VETA kwa kuweza kunipa  ujuzi huu, naishaurijamii isiweze kuwaficha wenye ulemavu,mimi nlikuwa sina ujuzi wowote lakini baada ya kufika VETA nimekuwa fundi ambaye naweza kushona nguo ya aina yoyote. Napenda niiase jamii kuwa hakuna kitu ambacho kinashindikana mimi leo hii ni mlemavu wa viungo lakini nilipokwenda kusoma VETA walinipokea vizuri wakanipa ushirikiano na hatimaye leo hii nimeweza kuwa fundi mzuri.

“Kama upo mtaani au kuna mtu yoyote mwenye changamoto ya ulemavu kama mimi mlete VETA wala msimfiche kwasababu ukifika utakutana na viongozi wenye uwezo wa kutambua huyu mwenye changamoto hii tumuweke kwenye fani gani, watakuchagulia fani inayoendana na wewe,” amesema na kuongezwa:

Alisema pia anamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwakuwekwaa   katika shule za ufundi stadi.

Riziki pia  ameiomba serikali kuweza kumpa ajira ya kuweza kushona sare za Jeshi la Polisi au Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Amesema tangu amalize chuo bado hajaweza kujiajiri kutokana na kutokuwa na mtaji hivyo anaiomba serikali iweze kumsaidia.

“Kujiajiri mwenyewe naweza changamoto ni mtaji. Lakini kama nitapata ajira nitashukuru zaidi hata kwenye taasisi ya Jeshi la Polisi au Jeshi la Kujenga Taifa nikajihusishe na mimi angalau kushona sare zao uwezo huo mimi ninao.

“Naiomba serikali iweze kunipa ajira kama ina uwezo huo, kama iliweza kuniamini ikanipokea VETA pamoja na ulemavu wangu, nina imani serikali yangu ni sikivu haiwezi kuacha kunipa ajira,” amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *