Jafo:Tutaendelea kuwalinda wafanyabiashara wa China ili kuzalisha ajira

Aziza Masoud,Dar es Salaam

SERIKALI  imesema itaendelea   kulinda uhusiano wa kibiashara na  wafanyabishara wanaotoka nchini China na nchi zote duniani wanaokuja  kuwekeza ili kuzalisha ajira hususani katika sekta binafsi.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Viwanda Dk.Suleimani Jafo katika manesho  ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasa wakati akizungumza katika mdahalo maalum wa siku ya China (China Day).

“Ofisi ya viwanda tunawakarobisha wote kutoka China na nchi mbalimbali kuwekeza,hususani katika kuleta ajira,wanaomaliza vyuo ni wengi kwa hiyo itakuwa ni sehemu ya kujiajiri katika sekta binafsi ,”amesema Jafo.

Amesema wizara kupitia taasisi ya Tantrade  wana dhamana  la kuwalinda wafanyabiashara hasa ukizingatia Taifa hilo lina mahusiano na Tanzania zaidi miaka 60.

“Leo ni China ambapo China na sisi tuna mahusiano zaidi ya maiak 60,tunafanya biashara na China zakusafirisha bidhaa zaidi ya Dola Za Marekani Bilioni 3.5,”amesema Jafo.

Amesema kampuni za China zimekuwa zikifanya kazi za ukandarasi  wakujrnga  miundombinu mbalimbali  nchini.

“Kampuni nyingi  za ujenzi zimetoka China, serikali imeweka  mazingira wezeshi ,ofisi ya viwanda tunawakaribisha wote kutoka China na nchi mbalimbali kuwekeza,”amesema Jafo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *