Na Aziza Masoud,Dar es Salaam
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandishi Felchesmi Mramba amesema Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) inafanya kazi nzuri ya udhibiti na kwamba wamefanikiwa kudhibiti bei ya umeme na kufanya nishati hiyo kuuzwa bei rahisi zaidi ukilinganisha na nchi za jirani.
Kauli hiyo ameitoa alipotembelea katika banda la Ewura lililopo katika maonesho ya 48 ya biashara y Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere,Mramba amesema taasisi hiyo ina wajibu wakudhibiti huduma za maji na nishati ambapo wanadhibiti huduma za umeme,gesi asilia na mafuta.
“Ewura inafanya kazi nzuri sana mpaka sasa hivi kama mnavyoona huduma zinadhitiwa pia zinapatikana na wameweza kudhibiti pamoja na upatikanaji wa huduma ,bei wamedhibiti pia ubora wa huduma hizo,nchi yetu ni miongoni mwa nchi yenye bei za chini sana ya huduma za umeme hata ukilinganisha na majirani,”amesema Mhandisi Mramba.
Amesema ubora wa nishati ya umeme umeimarika kwa sasa hata ukatikaji wa umeme sio sana na mgao umepungua.
“ Kukatika sana umeme vimeoungua hatusemi kama tupo vizuri lakini angalau tupo kwenye kiwango kinachoridhisha ,”amesema Mhandishi Mramba.
Amesema kwenye maeneo ya gesi asilia Ewura wamesaidia sana wanaendelea kufuatilia kutoa leseni kwa wanaojenga vituo hasa vya gesi asilia na mafuta.
“Wanasimamia kuhakikisha kuwa huduma zinazotolewana vitu vinakuwa kwenye ubora,sisi kama wizara ya nishati ni wajibu wetu kuhakikisha kuwa Ewura anafanya kazi yake kulingana na sharia na sera zilizopo pia tunamuwezesha kutekeleza majukumu yake katika mazingira rafiki ,”amesema Mhandisi Mramba.