Na Aziza Masoud,Dar es Salaam
MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Taifa la Bima (NIC), Abdi Mkeyenge amesema mkakati wa shirika kwa sasa ni kuifikia jamii na kuwapa elimu ya bima kwakuwa wananchi wengi hawana uelewa.
Mkeyenge ametoa kauli hiyo alipotembelea katika banda la NIC lililopo katika viwanja vya Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba,amesema wamegundua wananchi wengi hawana uelewa kuhusu bima hivyo wanaona ni kama kitu ambacho si cha muhimu.
“Mikakati ambayo tumeweka sasa hivi ni kutoa uelewa kwa wananchi tutatoka tutaenda tutaeleimisha kuhusu bidhaa na huduma tunazotoa .
“Tumegundua elimu ya bima Tanzania ipo chini kabisa,unakutana na mtu anakwambia bima ya nini ,sisi sasa tunakuja na mkakati wa kuelimisha jamii na kutoa mafunzo,bima ni muhimu na uwezi kuona umuhimu wake kama hayajakukuta sasa hatusubiri yakukute tutahikikisha elimu inamfikia kila mmoja ili waweze kujiunga na Bima,“amesema Mkeyenge.
Amesema watawawezesha wafanyakazi mafunzo hawa wanaofundisha kuwawezesha wafanyaka kupata mafunzo ya muda mfupi mfupi ili waweze kuwasilisha kwa wananchi.
Mbali na hilo Mkeyenge pia amewataka wawekezaji nchini kukata bima za biashara zao ili pindi majanga yanapojitokeza waweze kufidiwa kwa wakati na kuendelea kuzalisha.
“NIC hili ni shirika la umma hivyo tunatoa bima aina mbili za maisha na zisizo za maisha ambazo hizi zinawagusa moja kwa moja wawekezaji kwani mwekezaji akipata majanga tunaweza kuwafidia na wakaendelea na uwekezaji wake kama kawaida na kufanya nchi iweze kuendelea kwa uchumi “,amesema.
Amesema pamoja na kuwa uni Taasisi ya serikali lakini pia wanafanyabishara kwani wanajukumu la kulipa kodi lakini wanajukumu kubwa la kuwahudumia Watanzania.