Na Aziza Masoud,Dar es Salaam
MAMLAKA ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imesema moja kipaumbele chao ni kuhakikisha wanaongeza wawekezaji kwenye utafutaji wa gesi
kwa lengo la kuongeza matumizi ya gesi asilia viwandani na majumbani.
Akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kitaifa ya Dar es Salaam (DITF) Mwenyekiti wa bodi ya Wakurungezi PURA, Halfani Halfani alisema kwa kipindi kirefu kumekuwa hakuna uwekezaji wakutosha na maeneo mengine hayana uwekezaji.
“Kisheria wamerudisha yale maeneo serikalini hivyo tuna jukumu lakutafuya wawekezaji ili kutekeleza hilo,taasisi imekuwa inafanya matayarisho ya sheria,sheria ndogo inaelekeza wawekezaji watafutwe kwa ushindani sio kwakuokotwa hapana,”
“Ili wapatikane kwa ushindani wanafanya mikutano yakutangaza marneo wawekezaji wanakuja wanasikiliza na wanaleta propasal (dokezo) wa hayo maeneo,”amesema Halfani.
Amesema zoezi hilo huenda linaweza likafanyika robo ya kwanza ya mwaka ujao
Alisema sheria ya mafuta inaelekea ni kazi ya waziri ni kutoa leseni yeye ni mtoa leseni hivyo anamwaga sera kama serikali alafu watalaam wanachukua jukwaa wanasema maeneo yaliyopo na masharti alafu itaamua nani atapata kitalu.
“Maeneo ambayo yapo yanayozalisha gesi mpaka sasa Songosongo wilaya ya Kilwa na Mnazi Bay wilaya ya Mtwara vijijini lakini mwaka huu serikali imetoa leseni ya uendelezaji ya pamoja kwa sababu ni uzalishaji,imetoa kwa leseni kwa muwekzaji mmoja mwenye asili yakiarabu,”amesema.
Amesema mzalushaji huyo anategemewa kuanza kuzalisha gesi mwakani hivyo sasa hivi atafanya matayarisho ya mwisho ambayo ni ujenzi wa bomba kutoka eneo la kisima mpaka kwenye mitambo yakusafisha gesi Madimba.
“Tunategemea atakuwa na uwezo wakuzalisha takribani futi za ujazo milioni 100 kwa siku kiasi ambacho kinaweza kuongezeka kadri gesi inavyoweza kuzalishwa na kadri visima vitakavyofanya kazi .
“Huyu muwekezaji atakavyoanza kuzalisha tutegemea na hali ya uzalishaji kwa sababu kwa kipindi cha muda mrefu tulikuwa tunategemea gesi ya baharini na gesi ya pale Lindi watatupatia zaidi kwa ajili ya matumizi ya majumbani,”amesema.
Amesema pamoja kwamba na watakuwa wanauza lakini kuna kiasi fulani watatakiwa kukiacha hapa nchini .
“Hiyo ni kazi ya Pura kuhakikisha kunakuwa na ulinzi wa usambazaji,kama Pura tutajipanga vizuri ni lazima kuhakikisha hatutakuwa na uhaba wa gesi ,”amesema.
Mwisho