NIC yawaalika wawekezaji wenye miradi mikubwa kukata bima 

Na Aziza Masoud,Dar es Salaam

SHIRIKA la Bima laTaifa (NIC) limewashauri  wawekezaji ambao wanakuja kutekeleza miradi mikubwa nchini kukata  bima inayohusu uwekezaji  ili waweze kufanya shughuli zao bila hofu. 

NIC imetoa kauli hiyo jana wakati wa kilele cha maazimisho ya Maonesho ya  48 ya Biashara maarufu kama Sabasaba ambapo pia walifanikiwa kupata tuzo ya mshindi wa kwanza iliyotolewa na Mamlaka ya BiasharaTanzania  (Tantrade) katika kundi la watoa huduma kwa maana ya  kampuni bora ya bima katika maonesho hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada yakupokea tuzo hiyo Mkurugenzi Mkuu wa NIC,Kaimu Abdi Mkeyenge amesema  shirika kongwe la serikali ambalo limekuwa likitoa huduma za bima mbalimbali ikwemo katika  katika miradi  mikubwa ya uwekezaji inayotekelezwa nchini  ambapo  zipo bima hadi za viashiria vya hatari.

‘Tunaweza kumkatia bima ya  viasharia ambavyo ni vibaya kwa maana ya viatarishi mwekezaji ,tunaweza kufanya management na programu nzuri kwa ajili ya miradi mikubwa, kwa ajili ya biashara kwa sababu biashara  ina viatarishi vingi.

‘Inawezekana kabisa wawekezaji wakawa na hofu na nchi yetu kwa kudhani kuwa  hakuna taasisi kubwa ambayo inaweza kukata bima  kwenye miradi mikubwa,hofu hii waiondoe mfano tu tunakata bima katika miradi mbalimbali kama ya bwawa la Nyerere (Bwawa la Julius Nyerere) ambalo  linazalisha umeme ,mradi wa reli ya kisasa (SGR) na miradi mingine mingi ,’amesema Mkeyenge.

Amesema wawekezaji wengi ambao wanategemewa  kutoka nje ya nchi kuja kuwekeza wanapaswa kujua wapo salama  kwakuwa NIC  kama wakata bima na watoa  huduma za bima wanahusika moja kwa moja katika kusaidia wafanyabiashara au wawekezaji kufanya shughuli zao salama.

Amesema mbali na miradi hiyo NIC pia inakata bila katika miradi ya nishati hasa katika kipindi hiki ambacho Tanzania imeanza kuvuna gesi .

‘Tupo hapa kwa ajili yakuweka mazingira salama ya ufanyaji kazi na biashara ili tuweze kuchangia mchango wa uchumi katika Taifa letu,’amesema Mkeyenge.

Amesema NIC pia inatoa bima za maisha ambazo zinaweza kuwapatia wananchi maisha salama,bima za kilimo ,bima za mitambo kwa wale wenye kampuni na wanazalisha ,bima za vifaa vya nyumbani,bima za nyumba,bima za vifaa vya moto yakiwemo magari madogo na  makubwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *